Saturday, January 16, 2021

Wema: Mimi ni Miss Tanzania milele

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA JOSEPH SHALUWA, MWANZA

STAA wa filamu Bongo, Wema Issac Sepetu ambaye ni zao la Miss Tanzania mwaka 2006, ametamba kuwa yeye ni Miss Tanzania milele kauli iliyoibua shangwe kubwa ukumbini.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Viwanja vya Rocky City Mall, jijini hapa kulipokuwa na Fainali za Miss Tanzania mwaka 2016 ambapo Diana Edward (18) kutoka Kinondoni aliibuka mshindi.

Wema alipanda jukwaani baada ya kuitwa na mwanamuziki, Christian Bella, aliyekuwa akitumbuiza jukwaani, alipopewa maiki aseme chochote, akafunguka hayo.

“Nilimwambia mdogo wangu, Lilian Kamanzima, wakati akitoa speech hapa, asisasahau kusema kuwa ukiwa Miss Tanzania, unaendelea kuwa hivyo milele. So mimi ni Miss Tanzania 2006, hakuna mwingine tena kwa mwaka huo.

“Najivunia hilo kwa kweli na mamisi wote tunapaswa kujivunia kwa hilo. Ninawatia sana moyo wadogo zangu wanaochuana leo na mwisho, lazima mmoja aibuke mshindi,” alisema Wema ambaye pia anajulikana kwa jina la Madam.

Kabla ya kupanda jukwaani, Wema alisogea mbele ya jukwaa na kuanza kumtuza Bella noti za elfu kumikumi, ndipo akamwita juu ambapo kabla ya kufanya chochote aliendelea kumtuza kwanza.

“We’ Bella nilikuwa sijamaliza kukutuza, ngoja nimalizie kwanza kukutuza halafu nikusikilize,” alisema Wema akidondosha noti nyekundu-nyekundu.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -