Saturday, November 28, 2020

A.J VS KLITSCHKO LITAKUWA PAMBANO LA KITAJIRI ENGLAND

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

PAMBANO la milioni 42 kati ya Anthony Joshua na Wladimir Klitschko, litakuwa la kitajiri kuwahi kutokea England.

Bingwa huyo wa mkanda wa IBF atakumbana na bondia wa Ukraine, mwenye umri wa miaka 40, huku mkanda uliowazi wa WBA nao utawaniwa kwenye pambano hilo linanalotarajiwa kufanyika Aprili 29, mwakani katika Uwanja wa Wembley.

Pambano hilo linatarajiwa kuvunja rekodi ya pauni milioni 22 iliyowekwa na bondia Carl Froch na George Groves, mwaka 2014.

Joshua, mwenye umri wa miaka 27, anatarajiwa kulipwa zaidi ya kile alichokuwa akilipwa kabla kwa ajili ya kutetea taji lake la IBF kwa mara ya tatu, baada ya kumdunda Eric Molina mwishoni mwa wiki iliyopita.

Pambano la Froch na Groves liliingiza mashabiki 80,000 katika Uwanja wa Wembley, lakini promota wa Joshua, Eddie Hearn, ana uhakika wa Meya wa London na ataruhusu mashabiki 90,000 kuingia uwanjani.

Pambano hilo litazalisha pauni milioni 8 kwa watu watakaolipia kuangalia nyumbani, ambapo pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao, mwaka jana lilinunuliwa na watu milioni 1.15 kuangalia pambano hilo.

Pambano hilo la Joshua dhidi ya Klitschko linaaminika linaweza likanunuliwa kwa pauni milioni 1.5, ambapo ikitarajiwa kuingiza pauni milioni 25.4.

Televisheni ya RTL italipa pauni milioni 4 kwa ajili ya kuonyesha pambano hilo kwenye televisheni za Ujerumani, televisheni za Marekani watatoa pauni 1.5 kwa ajili ya kipindi cha Showtime au HBO kupata haki ya kuonyesha pambano hilo, huku televisheni nyingine zikitarajiwa kununua kwa pauni milioni 1.

Fedha za wadhamini huenda ikawa ni pauni milioni moja kwa makampuni ambayo yameshaahidi kudhamini.

Fedha hizo zote hazijajumlishwa na zile za wadhamini wa AJ, Under Armour, Beats By Dre, Lucozade, StubHub, Jaguar, EQ Nutrition, Dafabet na Lynx ambao wanamlipa mshindi wa medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki mwaka 2012.

Pauni milioni 1 zinatarajiwa kuchangishwa kuweza kufikia pauni milioni 42 kwa ajili ya pambano hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -