Sunday, January 17, 2021

ACHA FIKRA HIZI POTOFU, MWELEWE ANAPOKUKATAA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

KUNA baadhi ya watu wanalaumu wenzao katika mahusiano, ila ukiangalia kwa makini wao ndio wenye kustahili lawama. Angalia, unamtongoza msichana halafu anakwambia ana mtu – unakasirika. Kibaya zaidi unaanza kumpakazia kuwa ni msichana malaya asiyefaa na mengineyo mengi. Kisa? Kakukatalia!

Ulitaka afanye nini? Akukubalie ilhali akijua ana mtu tayari? Au ulitaka akwambie hana mtu? Baada ya kuwa na wewe katika mahusiano na ukigundua anaye itakuaje? Kati yake na wewe nani asiyefaa hapo? Kutokana na hali hii ya ujinga wa baadhi ya wanaume, wanawake wajinga wakikutana nao wao wanawakubalia tu.

Akukatalie ili uanze kumpakazia? Maana wengine akili ndiyo hawana kabisaa, wakikataliwa wanataka kumjua hadi bwana wa msichana husika na wakimjua tu kosa. Kazi anayo, habari chafu za ukweli na uongo zinazomuhusu msichana wake zote watampatia.Eti kwa madai wanamkomoa? Umkomoe kwa kosa gani?  Siyo ulimbukeni huo?

Msichana kukukatalia hata kama hana bwana si kosa. Mapenzi ni hisia! Kama hana hisia na wewe ajilazimishe? Haiwezekani! Ni lazima akukatae tu.

Anaweza kukubali kwa kuwa anakuogopa utamfanyia kitu mbaya kutokana na sifa yako inayovuma mtaani ila jua hawezi kuwa mpenzi bora kwako. Hawezi kufanya yale yanayotakiwa kufanywa na wapenzi. Wenye akili finyu utasikia wakisema: Ila nikitaka si ananipa? Ndiyo, anaweza kukupa sasa hayo ndiyo mapenzi?

Kama shida yako ilikuwa hiyo tu, si mara mia ungeenda kwenye madanguro maana hata husumbuki kuchosha mdomo ni hela yako tu! Nisieleweke vibaya kuhusiana na hili, lengo si kuhamasisha ukahaba ila ni kutaka kukuonesha thamani ya mapenzi kuwa haipataikani kati kati ya mapaja ikiwa hakuna hisia na maridhianao baina ya wahusika. Katika maisha kila kitu kina sababu zake.

Kama hataki uwe mapenzi wake omba urafiki muweze kuzungumza mambo mengine ya kimaisha. Maisha hayaishii katika mapenzi . Fungua fursa zingine baada ya kushindwa ombi la kwanza. Kumnunia au kumchukia anayekukataa ni ujinga.  Wanaofurahia mapenzi ni wale ambao kila mmoja bila kulazimisha kwa chochote waliridhiana.

Ndiyo maana leo unawaona hivyo. Wanafurahi pamoja, mmoja akipata tatizo mwenzake anajitolea kwa hali na mali kuweza kumsaidia. Wanapigiana simu bila kulazimishana, maneno matamu midomoni mwao hayakauki. Yote hayo ni kwa sababu wanapendana na wameridhiana kuwa pamoja.

Mtu ambaye amekuwa na wewe bila kushurutishwa na vitisho vyako ndiye pekee anayeweza kukufanya ukafurahia mapenzi. Wakati mwingine ni vyema ukapata muda wa kujiuliza kwanini unakuwa na mtu kimahusiano. Ni kwa kuwa unataka amani na raha ya kuwa na yule umpendaye? Au ni kwa kuwa unataka f’lani na f’lani wajue na wewe upo katika mahusiano?

Yote kwa yote tunapaswa kujua mapenzi siyo ‘fashion’. Mapenzi si ya kuangalia unavyoonekana au unavyotembea ndiyo upendwe. Hapana. Hata kama una nini, kama kasema hakupendi heshimu uamuzi wake. kumkasirikia kwa kitu ambacho si kosa lake ni uwendawazimu. Hisia huja zenyewe tu, si suala la kuzilazimisha. Kama angekuwa anahisia na wewe wala isingehitaji lazimisho lolote kutoka kwako ili aweze kukukubali. Mwenyewe tu!

Mapenzi yanapotamalaki katika nafsi ya mtu hujikuta akifanya kila liwezekanalo aweze kuwa na wewe. Ukiona kila jitihada unazofanya juu ya kumpata hazizai matunda jua hana hisia na wewe. Ulie ucheke ukweli utabaki pale pale. Hakupendi. Sasa kwanini umpakazie mambo machafu eti kisa amekukataa? Ni ujinga!

 ramadhanimasen@gayahoo.com 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -