Friday, January 15, 2021

Achana na ubingwa! ‘Top Four’ yenyewe ni vita kali EPL

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

TANGU kuanza kwa msimu huu wa 2016-17, macho na masikio ya mashabiki wengi wa klabu za Ligi Kuu England yameelekezwa kwenye mbio za kuwania ubingwa tu.

Eti! Wengi wao wanaamini utamu wa ligi hiyo maarufu duniani upo kwenye taji hilo tu. Kitu ambacho hawajagundua ni kwamba mbali ya ubingwa kuna vita kali ya kuwania nafasi nne za juu.

Ikumbukwe ni kuwa timu nne za juu hupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, hivyo kuna ushindani mkubwa katika kujihakikishia ‘Top Four’.

Mpaka sasa, kwa mujibu wa msimamo wa Ligi Kuu England msimu huu wa 2016-17, timu tano zina uhakika wa kumaliza mbio za ubingwa zikiwa nafasi nne za juu.

Ikumbukwe kuwa, ni mechi tisa pekee zimechezwa tangu kuanza kwa msimu huu huku bingwa mtetezi akiwa ni Leicester City.

Lakini pia, ni pointi moja pekee inayozitenganisha timu hizo zinazoshika nafasi tano za juu.

Manchester City walioko kileleni wamejikusanyia pointi 20 na wameonekana kukamia msimu huu wakiwa chini ya kocha mpya Pep Guardiola.

Ni ngumu kuamini kuwa Man City watamaliza ligi wakiwa nje ya timu nne za juu ikiwa Sergio Aguero atakuwa fiti.

Lakini pia, uwepo wa Kevin De Bruyne na kinda Raheem Sterling ni faida kubwa kwa matajiri hao wa jijini Manchester City.

Pia, kutokana na uwepo wa Guardiola ambaye mafanikio yake katika klabu zote alizofundisha yako wazi, ni rahisi kuamini kuwa hata Man City wakikosa ubingwa basi hawawezi kutupwa nje ya Top Four.

Anachotakiwa kukifanya Guardiola ili Man City ipate nafasi hiyo ni kuboresha safu yake ya ulinzi.

Anachotakiwa kukifanya Guardiola ni kuboresha safu yake ya ushambuliaji. Kwa kiasi kikubwa, bado beki John Stones na mlinda mlango Claudio Bravo wameshindwa kuthibitisha kile kilichofanywa wasajiliwe. Kwa upande mwingine, Guardiola haonekani kuukubali uwezo wa mkongwe Vincent Kompany.

Wenzao Arsenal wanashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England wakiwa wamejikusanyia pointi 20. Kama hujui, wanachotambia Arsenal msimu huu ni uimara wa safu ya kiungo na kipa Petr Cech.

Ni wazi itashangaza kuiona Arsenal ikimaliza ligi bila kuingia nafasi nne za juu. Alexis Sanchez na Theo Walcott wamefufuka na kuwa sehemu muhimu ya kikosi cha mzee Arsene Wenger.

Kwa miaka mingi, Arsenal wakipotezwa na wimbi la majeruhi. Kama msimu huu hawatokumbwa na majanga hayo, kuna uwezekano mkubwa wa kuchukua ubingwa na kama watalikosa taji hilo basi hawatokuwa nje ya Top Four.

Ukiachana na wakali hao wa Kaskazini mwa London, Liverpool wanaokamata nafasi ya tatu kwa pointi zao 20, hawawezi kupuuzwa kwenye mbio za kupigania nafasi nne za juu.

Hakuna ubishi kuwa uimara wa kikosi hicho cha kocha Jurgen Klopp unategemea uzima wa Philippe Coutinho na Roberto Fiminho.

Hata hivyo, hawapaswi kuwategemea sana viungo katika jukumu la kupachika mabao. Ingekuwa poa kama Klopp angelikabidhi jukumu hilo kwa Daniel Sturridge.

Kwa upande wa pili, unawezaje kuinyima Chelsea top four? Ni ngumu hasa kutokana na ubora waliouonyesha tangu kuanza kwa msimu huu.

Mpaka sasa, matajiri hao wa Magharibi mwa London wamejikusanyia pointi 19 na wanashika nafasi ya nne.

Tangu alipoanza kutumia mfumo wa 3-4-3, kocha Antonio Conte hajapata machungu ya kupoteza mchezo. Eden Hazard amerejea kwenye ubora wake huku N’Golo Kante akiwa ‘on fire’.

Tottenham wanaoshika nafasi ya tano wamejikusanyia pointi 19 na wana uhakika mkubwa wa kumaliza ligi wakiwa Top Four.

Falsafa ya kushambulia kwa kasi ya kocha Mauricio Pochettino ndiyo siri ya mafanikio ya timu hiyo msimu uliopita.

Wameonekana kuimarika zaidi msimu huu kutokana na kombinesheni kali ya safu ya ulinzi ya Toby Alderweireld na Jan Vertonghen huku safu ya kiungo ikishikiliwa na Mkenya Victor Wanyama.

Kama si ubingwa, ili kujihakikishia nafasi nne za juu, Spurs wanatakiwa kuhakikisha Harry Kane anarejea kwenye ubora wake wa kuwatungua walinda mlango.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -