Tuesday, October 27, 2020

Acheni kuchonga……Mourinho awabwatukia wapondaji

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Manchester United, Jose Mourinho, ameibuka na kusema kuwa mpira wa sasa umejaa uchochezi ‘usio na maana’, kila mtu akijifanya anajua kukosoa baada ya timu yake kutokuwa na mwenendo mzuri katika michezo yao ya hivi karibuni.

Mourinho aliwaelezea wale wanaoijadili timu yake kuhusu kiwango hafifu walichonacho kwa sasa akitumia jina la mwanafalsafa wa zamani wa sayansi, Albert Einsteins, aliyevumbua mifumo mbalimbali ya kisayansi, hasa kwenye somo la fizikia.

“Tuna mechi tatu za nyumbani zinazokuja, ni vizuri sana kuwa nyumbani,” alisema Mourinho, alipozungumza na gazeti la Manchester Evening.

“Naelewa masikitiko yaliyopo, kama mashabiki wamesikitishwa na wiki iliyopita naelewa kabisa, lakini nina uhakika bado wataibeba timu kama kawaida yao.

“Tulikuwa na wiki mbaya sana. Dunia imejaa watu kama ‘Einsteins’, najua wamejaribu kufuta miaka 16 ya taaluma yangu, wamejaribu kufuta historia nzuri ya klabu ya Manchester United, huku wakiiangalia wiki hiyo moja iliyokuwa na matokeo matatu mabaya. Lakini huo ndo mpira mpya uliojaa watu wenye akili nyingi,” aliongea kocha huyo.

United ilimaliza gundu la kupoteza mechi tatu mfululizo kwa kuwafunga Northampton mabao 3-1 kwenye mchezo wa kombe la ligi ya England na kupangwa na wapinzani wao wa jadi, Manchester City, kwenye mzunguko wa nne wa michuano hiyo.

Kabla ya mtanange huo utakaopigwa Oktoba mwaka huu, United wanatarajia kucheza mechi ya Ligi Kuu England dhidi ya mabingwa watetezi, Leicester City, wikiendi hii katika uwanja wa Old Trafford.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -