Monday, November 23, 2020

Adebayor amefeli soka akafaulu maisha

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LONDON, England

HIVI karibuni, staa Emmanuel Adebayor, mwenye umri wa miaka 32, alikaribia kabisa kutua katika klabu ya Lyon, lakini kocha wao, Bruno Genesio, alisitisha mpango huo katika dakika za mwisho.

“Kuna sehemu ambayo huwa tunapata msosi, hivyo nilitaka kukutana naye (Adebayor) ili tupate kahawa,” alisema Genesio, alipokuwa akihojiwa na mtandao wa Sun.

“Lakini, kilichonishangaza, alipofika alitaka kahawa yake ichanganywe na ‘whisky’ (aina ya pombe). Pia, alikuwa na sigara mdomoni. “Kilichonijia kichwani ni kwamba hana nafasi kwenye klabu yetu.”

Itakumbukwa kuwa, baada ya kutemwa na Crystal Palace mwishoni mwa msimu uliopita, nyota huyo raia wa Togo amekuwa nje ya mfumo rasmi wa soka.

Lakini pia, hata Palace watakiri kuwa walicheza kamari tu kumsajili Adebayor, kwani tayari alikuwa nje ya soka la ushindani kwa kipindi kirefu baada ya kuondoka Tottenham.

Mara kadhaa, ‘tozi’ huyo alinaswa na kamera za waandishi wa habari akiwa barani Afrika akitanua, huku akiutumia muda huo ‘kuposti’ picha kwenye mitandao ya kijamii zikionesha mali anazomiliki, yakiwemo magari yake ya kifahari.

Kwa kipindi chote alichokaa Palace, mkali huyo alifunga bao moja pekee, jambo lililowafanya mabosi wa klabu hiyo kumfungashia virago, hakuwa na jipya zaidi ya kuibuka mazoezini na ‘style’ mbalimbali za nywele na mavazi.

Wakati wa dirisha la usajili la majira haya ya kiangazi, staa huyo mwenye umri wa miaka 32 alihusishwa na mpango wa kutua Fulham, lakini dili hilo liliota mbawa.

Baadaye taarifa zilimtaja Adebayor kwenye mpango wa kutua Kaskazini mwa Jiji la London na kujiunga na klabu yake ya zamani ya Totenham, lakini mpaka kufungwa kwa dirisha la usajili hakukuwa na lolote lililokuwa limefanyika.

Akizungumzia kuchemsha kwake kujiunga na Lyon siku chache zilizopita, straika huyo alisema klabu hiyo haikuchukulia ‘siriazi’ uhamisho wake.

Eti mpachikaji mabao huyo alidai kuwa klabu hiyo ya Ufaransa inatafuta visingizio tu kwa kushindwa kumsajili.

Vyanzo vingine vya habari vimedai kuwa sababu kubwa ya mabingwa hao mara saba wa Ligi Kuu Ufaransa kugoma kumsajili fowadi huyo ni kuporomoka kwa kiwango chake na wasiwasi wa kumkosa kwa takribani mwezi mmoja au miwili ikiwa atakwenda kuiwakilisha Togo kwenye Fainali za Mataifa za mwaka (Afcon 2017).

“Walijua wazi kuwa nitacheza kwenye mashindano hayo. Kama hiyo ndiyo sababu yao, watakuwa wanajimaliza wenyewe. Mimi ni nahodha wa nchi yangu, hivyo ni kwa namna gani nitaacha kwenda? Ingekuwaje kama Mfaransa angekaa kucheza michuano ya Euro?” alihoji Adebayor.

Katika hatua nyingine, staa huyo aliongeza kuwa alifika nchini Ufaransa mwishoni mwa wiki iliyopita kushughulikia uhamisho huo, lakini alishangazwa na maswali aliyokuwa akiulizwa na kocha wa Lyon.

“Nilifika Ijumaa asubuhi kuzungumza na kocha. Nilifikiri ilikuwa ni kufanyiwa vipimo na kusaini. Kocha aliniuliza maswali yaliyoniacha hoi. Alitaka kujua kama nimeoa na nina watoto,” aliongeza.

Adebayor alimwambia kocha huyo kuwa amekuwa akizichezea timu kubwa kwa miaka 15 na kukutana na makocha wenye majina makubwa kama Arsene Wenger, Jose Mourinho, Didier Deschamps na Roberto Mancini.

Hivyo, kwa kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza kucheza kwenye timu inayopambana kushuka daraja, hakupenda na ndiyo maana alishindwa kuwa kwenye kiwango cha juu.

Kwa upande mwingine, hata mashabiki wa Togo hawapaswi kutegemea makubwa kutoka kwa nyota wao hao wakati wa michuano ya Afcon kutokana na takwimu zake za uwanjani.

Licha ya kuwa nahodha na kiongozi wa safu ya ushambuliaji ya timu hiyo, nyota huyo alifunga bao moja pekee katika michezo yote ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2017 zitakazofanyika nchini Gabon.

Hata hivyo, nje ya uwanja, straika Adebayor anacho cha kujivunia kwa kipindi chote alichokitumia katika kusakata kabumbu.

Mkali huyo amejikusanyia utajiri unaotajwa kufikia Dola za Marekani milioni 27. Ikumbukwe kuwa, alipokuwa Manchester City, straika huyo alikuwa na uhakika wa kuvuna Dola za Marekani 268,000 kwa wiki.

Alipopelekwa Tottenham kwa mkopo akitokea kwa matajiri hao, Adebayor alikuwa akiweka mfukoni kitita cha pauni 170,000 kwa wiki.

Mbali na hilo, kutokana na klabu mbalimbali alizochezea barani Ulaya, ikiwemo Real Madrid, Adebayor amevuna mpunga mrefu katika mchezo wa soka.

Mwaka jana, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jarida maarufu la Forbes, nyota huyo ndiye aliyekuwa kinara kwenye orodha ya wanasoka wa Kiafrika wanaoingiza fedha nyingi, huku nafasi ya pili ikikamatwa na Asamoah Gyan wa Ghana.

Kutokana na hilo, ni wazi kuwa licha ya Adebayor kuonekana kutokuwa kwenye ubora wake wa kuzifumania nyavu uliompa heshima kubwa miaka ya nyuma, bado ni miongoni mwa waliofaidika na mchezo wa soka kutokana na kipato alichonacho hivi sasa.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -