Thursday, December 3, 2020

ADHABU YA BANDA YAPINGWA KILA KONA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA,

SIKU chache baada ya Kamati ya Saa 72 ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumsimamisha beki wa Simba, Abdi Banda, adhabu hiyo imepingwa kila kona na wadau mbalimbali wakihoji uhalali wa kamati hiyo kutoa maamuzi hayo.

Kamati hiyo ya saa 72 imemsimamisha Banda baada ya kumpiga ngumi nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila, kwenye mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita na klabu hiyo ya Msimbazi kulala kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Kutokana na kitendo hicho cha Banda, kamati hiyo ilikutana na kutoa maamuzi ya kumsimamisha Banda asicheze mechi yoyote hadi Kamati ya Nidhamu ya TFF itakapokaa na kumpangia adhabu nyingine kitu ambacho kimeonekana kuleta ukakasi kwa baadhi ya wadau.

Akizungumza na BINGWA, Mwanasheria Alex Mgongolwa, alisema kamati ya saa 72 iliundwa maalumu kukusanya matukio ya uwanjani ambayo hayahitaji uthibitisho wala hayana ulazima wa kumwita yeyote yule kwa maelezo hivyo uhalali wake unakuwa ndani ya saa hizo.

“Adhabu ya Banda imetolewa wakati tayari imeshapita zaidi ya siku saba na ile kamati inakuwa na uhalali ndani ya saa 72, ikishapita hapo kamati nyingine za TFF ndizo zinazohusika zaidi,” alisema Mgongolwa.

“Kamati hii pia haipaswi kusubiri uthibitisho au taarifa kutoka kwa nani au nani yaani kwenye maamuzi yake haimhitaji yeyote yule kwenye maamuzi yake kwa kuwa imeundwa kushughulikia matukio yote ya uwanjani. Kwa hiyo wamekosea kwenye maamuzi yao.

“Maamuzi yametoka jana (juzi), ila ukiangalia toka tukio hilo limetokea sasa hivi ni zaidi ya siku saba hivyo wamechelewa. Hili jambo lilipaswa kutolewa maamuzi mapema ila naiomba kamati ya nidhamu isichelewe kutoa adhabu kwa lengo la kulinda kiwango cha mchezaji.”

BINGWA lilimtafuta Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, ili kutoa ufafanuzi juu ya maamuzi hayo ambapo alisema shauri hilo limepelekwa kamati ya nidhamu kwa kuwa kosa hilo limejirudia.

“TFF ina kamati nyingi ila kamati ya mwisho ni ya rufaa, hivyo kamati ya saa 72 ilipogundua Banda ameshafanya kosa lile zaidi ya mara tatu ndio sababu ya kulihamisha kwenye kamati ya nidhamu ambapo hapo anaweza kukata rufaa,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -