Monday, January 18, 2021

AENDE TU, NI WAKATI WA WENGER KUPISHA WENGINE

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

LEO klabu ya Arsenal itaikaribisha Hull City kwenye dimba la Emirates katika mchezo wa Ligi Kuu England, mchezo ambao unatarajiwa kutoa matokeo tofauti na ya wiki iliyopita walipopoteza mechi mbili za ligi mfululizo na kufifisha matumaini yao ya kunyakua ubingwa msimu huu.

Matokeo hayo yalisababisha mashabiki kuanza kupaza sauti za kuchoshwa na mwenendo wa timu yao hiyo kwa kukosa taji la ligi kila msimu huku lawama nyingi zikimiminika kwa kocha, Arsene Wenger.

Mtandao wa Daily Mirror umegundua orodha ya siri ya makocha ambao wanaweza kutua Emirates, iwapo tu Wenger ataondoka majira yajayo ya kiangazi kama dalili zinavyoonesha kwamba huenda kocha huyo akaamua kufungasha virago vyake mara baada ya mkataba wake kufikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Orodha hiyo ya makocha wanne inaongozwa na kocha wa Borussia Dortmund, Thomas Tuchel, baada ya kufuatilia kwa kina ni kocha yupi mwenye uwezo wa kufundisha soka kwa kiwango cha hali ya juu.

Aidha, Max Allegri wa Juventus, Roger Schmidt wa Bayer Leverkusen na kocha wa Monaco, Leonardo Jardim, wamegundulika kuwa kwenye rada za Arsenal.

Umaarufu wa Mjerumani Tuchel barani Ulaya ni jinsi alivyoweza kuifanya Dortmund kucheza soka la kasi na lenye kuburudisha tangu aliporithi mikoba ya Jurgen Klopp.

Aidha, kocha huyo huenda akashawishika zaidi kuondoka Ujerumani ikiwa dili la Arsenal litawekwa mezani.

Mwitaliano Allegri pia inaaminika kuvutiwa na dili la kutua Arsenal (iwapo Wenger ataondoka), wakati huo Jardim naye yumo kwenye orodha hiyo kutokana na umaarufu aliojizolea hivi karibuni wa aina ya soka analofundisha, ambapo hadi sasa kikosi chake kimefunga mabao mengi Ligue 1 ya Ufaransa huku ikitesa kileleni mwa ligi hiyo.

Jardim ni mtu muhimu kwa mwenendo wa klabu yake ya Monaco hivi sasa, akifanikiwa kuifikisha hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo watacheza na Man City mwezi huu.

Huenda ukawa umeshtushwa kuliona jina la Schmidt, lakini ni kocha anayeheshimika Ujerumani kwa kuifanya Leverkusen icheze soka la kiushindani na kiwango kisichotetereka kila mara. Anahisiwa kuwa mmoja wa watakaopelekewa ofa mezani ya kuinoa Arsenal.

Majina ya makocha hao wanne ndiyo yanayotesa kwenye vyombo vya habari barani Ulaya kwa kuhusishwa na Arsenal, hasa baada ya kupitia kipindi cha kutakiwa kwa Eddie Howe wa Bournemouth ambaye kikosi chake kimeporomoka kiwango kwenye mechi za Ligi Kuu England.

Aidha, Ronald Koeman, alikuwa ni mmoja wa makocha walionaswa na rada ya Arsenal akiwa Southampton msimu ujao, kwa sasa yupo Everton na aina ya soka lake la fujo hataweza kutua Emirates.

Hata hivyo, mtandao wa Mirror unaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Wenger kusalia pale Emirates na kuna mkataba wa miaka miwili aliowekewa mezani.

Lakini kama ilivyoripotiwa wiki iliyopita, kocha huyo mwenye umri wa miaka 67, alifunguka wazi kwamba uamuzi wake wa mwisho utategemea na mwenendo wa Arsenal na nafasi watakayomaliza mwishoni mwa msimu.

Pia bodi ya klabu hiyo bado inampa ‘sapoti’ Wenger. Huku wakiwa hawaoneshi dalili ya kumpiga ‘panga’, hivyo mwenye uamuzi wa mwisho ni yeye mwenyewe.

Lakini licha ya hilo, wanatakiwa kuwa na mpango wa kutafuta mrithi wake muda wowote.

Inakumbukwa kuwa, Wenger aligoma kuzungumzia hatIma yake ndani ya klabu yake hiyo katika mkutano na waandishi wa habari mapema Alhamisi ya wiki hii, lakini inaonekana wazi kuwa makelele ya mashabiki yamemwathiri kufuatia vichapo viwili mfululizo kutoka kwa Watford na Chelsea.

Kwa sasa suala la kunyakua ubingwa mwaka huu ni kama ndoto na hesabu zinasema huu utakuwa mwaka wa 14 tangu Arsenal ilipotwaa taji la ligi kuu.

Je, Arsenal itafanikiwa kuishusha Chelsea kileleni kama Wenger alivyosema wiki hii kwamba msimu bado haujaisha? Tusubiri.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -