Monday, October 26, 2020

AFCON 2017: MICHUANO YA MATAIFA BINGWA KUANZA KESHO

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

Michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika, makala ya 31, itang’oa nanga Jumamosi saa 16:00 GMT (saa moja jioni Afrika Mashariki) pale wenyeji watakapokabiliana na Guinea-Bissau ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.

Miaka sitini imepita tangu kuchezwa kwa fainali za kwanza za kuamua Taifa Bingwa Afrika, ambayo ilichezewa nchini Sudan mwaka 1957.

Ni mataifa matatu pekee yaliyoshiriki na mshindi alikuwa Misri. Mwaka huu kutachezwa mechi 32 katika kipindi cha siku 23 na kushirikisha timu 16.

Michuano itaanza kwa hatua ya makundi, ambayo ni manne kila moja likiwa na mataifa manne. Mshindi atajulikana kwenye fainali tarehe 5 Februari na kupokezwa kikombe kilichoundiwa Italia pamoja na zawadi ya $4m.

Waafrika wanaendelea kuchangamkia michuano hiyo, ambayo bila shaka imeibuka kuwa kubwa zaidi ya soka barani Afrika.

Wenyeji Gabon wanaandaa michuano hiyo kwa mara nyingine miaka mitano tu baada ya kuwa mwenyeji kwa pamoja na Equatorial Guinea.

Walipewa fursa ya kuwa wenyeji baada ya kujiondoa kwa Libya kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Gabon ndilo taifa lililoorodheshwa chini zaidi orodha ya viwango vya soka ya FIFA mwezi Januari miongoni mwa timu zinazoshiriki, ambapo iliorodheshwa nambari 108.

Hata hivyo wana mchezaji nyota, Pierre-Emerick Aubamenyang anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani. Source BBC

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -