Tuesday, December 1, 2020

AFCON 2017 NI VITA YA MAKOCHA WANNE WAZAWA DHIDI YA WA KIGENI 12

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LIBREVILLE, Gabon


UKIWA ni takribani mwaka mmoja tangu aliyekuwa kocha wa timu Taifa ya Nigeria, marehemu Stephen Keshi aage dunia, mambo bado yanaonekana kutobadilika katika michuano ya fainali za Mataifa ya Afrika Afcon 2017.

Hii ni kutokana na kwamba, bado idadi ya makocha wa kigeni wanaonekana kupewa nafasi kubwa ikilinganishwa na wazawa.

Keshi alitoa lawama kuhusu jambo hilo la kutothaminiwa makocha wazawa  wakati Nigeria ikijiandaa kuivaa Mali  katika mechi ya nusu fainali ya michuano ya mwaka 2013 iliyofanyika nchini Afrika Kusini na aliyalaumu  mashirikisho ya soka Afrika kwa kuteua makocha kutoka Ulaya bila sifa za kutosha.

“Huwezi kumleta kocha kutoka Ulaya kisha ukanieleza kwamba ni bora kuliko mimi, sitakubaliana na hilo,” alisema Keshi ambaye alikuwa nahodha mwaka 1994 na kisha kocha mwaka 2013.

Pamoja na lawama hizo za Keshi ambaye alifariki mwaka jana, mambo yanaonekana kuwa hayajabadilika.

Hali hii ni kutokana na kwamba wakati timu 16 zikijiandaa na michuano hiyo itakayofanyika nchini Gabon ni makocha wazawa wanne pekee ambao wataziongoza timu zao za taifa.

Mokocha hao ni Aliou Cisse ambaye ataiongoza Senegal na Florent Ibenge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Cisse ambaye ni nahodha wa zamani wa Simba hao wa Terranga, anarejea kwenye michuano hiyo ya wanafainali wa mwaka 2002 akiwa kama kocha wakati Ibenge aikiwa mshindi na DRC baada ya kuiongoza Leopards kutwaa ubingwa wa michuano kama hiyo, lakini kwa wachezaji wanaocheza soka la ndani Chan mwaka mmoja uliopita.

Makocha wengine ambao majina yao hayafahamiki ni wa Guinea Bissau,  Baciro Cande na Wazimbabwe, Callisto Pasuwa.

Katika orodha hiyo makocha kati ya 16, 13 wanatokea Ulaya ambapo Ufaransa ndiyo inayoongoza ikiwa na makocha wanne wakiwa ni wawili zaidi dhidi ya Ubelgji na mmoja zaidi dhidi ya Israel, Hispania, Poland na Serbia.

Kwa upande wa Amerika Kusini ambao unasifika kubeba vipaji vya soka, wao wana kocha mmoja ambaye ni Muargentina, Hector Cuper, atakayekuwa akiwaongoza mabingwa  mara saba Misri.

Utamaduni huo wa kutegemea makocha wa kigeni badala ya wazawa unaonekana ni wa muda mrefu na una ushawishi mkubwa katika soka la Afrika.

Hali hiyo ni kutokana na kwamba kocha kutoka Hungary, Pal Titkos, ndiye aliyeiwezesha Misri kutwaa ubingwa mwaka 1959 yakiwa ni mashindano ya pili tangu michuano hiyo ianze na tangu kipindi hicho imeweza kuongeza mengine sita.

Katika mashindano yote hayo makocha wa Kiafrika wamefanikiwa kunyakua ubingwa mara 13 wakati wa kigeni wamefanya hivyo mara 16 yakiwamo yaliyopita ambayo kocha Herve Renard alitwaa taji hilo akiwa na Ivory Coast.

Ifuatayo ni orodha ya makocha watakaokuwapo Afcon 2017

Kundi  A: Gabon – Antonia Camacho (Hispania), Burkina Faso – Paul Duarte (Ureno), Cameroon – Hugo Broos (Ubelgji) na Guinea Bissau – Baciro Cande (Guinea Bissau.

Kundi  B: Algeria – George Leekens (Ubelgji), Tunisia – Henryk Kasperczak (Poland), Senegal – Aliou Cisse (Senegal) na Zimbabwe – Callisto Pasuwa (Zimbabwe).

Kundi  C: Ivory Coast – Michel Dussayer (Ufaransa), DR Congo – Florent Ibenge (DR Congo), Morocco (Herve Renard) na  Togo – Claude Re Loy (Ufaransa).

Kundi  D: Ghana – Avram Grant (Israel), Mali – Alain Giresse (Ufaransa), Misri, Hector Cuper (Argentina) na  Uganda – Mulitin Sredojevic (Serbia).

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -