Monday, October 26, 2020

AFCON 2019 TUSIPOANGALIA TUTAWAKILISHWA NA ALI KIBA AU DOGO JANJA

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA EZEKIEL TENDWA

RATIBA ya kutafuta kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mwaka 2019 itakayofanyika nchini Cameroon, imeshatoka na Tanzania imeshajua itakaokutana nao kwenye kundi L ambalo ndilo walilopangiwa.

Katika kundi hilo, timu yetu ya Taifa ‘Taifa Stars’ imepangwa sambamba na Cape Verde, Lesotho pamoja na Uganda ambao kwa bahati nzuri wao watashiriki michuano ya mwaka huu nchini Gabon.

Wakati wenzetu Uganda wakiwakilishwa na timu yao ya Taifa, sisi Watanzania hakuna jingine la kujivunia zaidi ya kusubiri muda wa ufunguzi tumwangalie msanii wetu wa kizazi kipya, Nasibu Abdul ‘Diamond’, namna atakavyotumia vizuri kipaza sauti akiimba.

Ni aibu badala ya kujisifu na timu yetu ya Taifa tupo macho juu tukijisifu na uwakilishi wa Diamond na hapo ndipo unapotokea utofauti kati ya soka la Tanzania na lile la wenzetu. Hapa tumezoea ujanja ujanja tu.

Uzuri wa waandaaji wa michuano hii huwa wanatoa ratiba mapema na kuwaachia washiriki kupima wenyewe namna ya kujiandaa na kama kawaida sisi maandalizi yetu yamekuwa ya kulipua, huku Shirikisho la Soka nchini (TFF), wakileta siasa nyingi badala ya kuangalia namna ya kuliongoza soka.

Mfano mzuri ni kwamba, baada ya ratiba hiyo kutoka utaona mpaka mashindano yanafika karibu ndiyo TFF wataanza maandalizi na hiki ndicho kitakachoendelea kutuangusha na si kwamba viongozi wetu hawajui. Wanajua sana ila kwa sababu wanaonekana hawana mipango endelevu wanabakia kupiga hatua moja mbele, nne nyuma.

Nina wasiwasi mkubwa kwamba kama katika Afcon ya mwaka huu inayoanza kutimua vumbi lake leo Gabon tutawakilishwa na Diamond, hiyo ya 2019 nchini Cameroon, tunaweza kuwakilishwa na msanii mwingine na bahati hiyo inaweza kumwangukia Dogo Janja au Ali Kiba. Hakuna namna.

Kocha wa Stars aliyepita, Charles Mkwassa, ni moja ya makocha wazuri tuliobahatika kuwapata katika nchi yetu lakini kutokana na ubabaishaji uliokithiri pale TFF, kufumba na kufumbua tukashangaa hajaongezewa mkataba na nafasi yake akapewa Jackson Mayanga.

Soka letu haliendelei kwa sababu limejaa viongozi walevi wa madaraka ndiyo maana kila kukicha tunazidi kusikia matukio ya kushangaza Ligi Daraja la Kwanza, ambapo tatizo kubwa linalotajwa ni kwamba kuna timu ziliahidiwa kupandishwa daraja sasa mipango inafanyika kwamba wawe na uwezo au hawana lazima wapande. Hii inapatikana Tanzania peke yake.

Kwenye chaguzi za mikoa ndiyo usiseme kabisa ni vurugu mtindo mmoja, kwani kiongozi anayekubalika na wengi utashangaa anapigwa chini na anapewa yule ambaye uwezo wake ni kupiga kura tu, sasa kwa hali hii tutarajie kuiona Stars ikicheza Afcon 2019 au tutawakilishwa na akina Saida Karoli?

Wakati tunalichambua kundi ambalo Stars wamepangwa, mwenzangu Hussein Omary, alidiriki kusema tukishindwa kufanya vizuri hapa sasa ni wakati wa kugeukia michezo mingine, kwamba soka limeshindikana kabisa na mimi sikumbishia.

Cape Verde si timu ya kutisha hata kidogo, hao Lesotho nao wala si watu wa kutulaza macho na pia Uganda licha ya kwamba wapo kwenye michuano inayoanza leo Gabon, lakini ni ndugu zetu tunaojuana ndani nje hivyo kama tutajipanga mapema tunaweza kupiga hatua moja mbele.

Kwa sababu ratiba imeshatoka inatakiwa akili zinanze kuchanganya kuanzia sasa, kocha mkuu apewe kila anachokihitaji japo namhurumia sana Mayanga, kwani anaweza akanyimwa fursa hiyo na timu ikifanya vibaya lawama zote akatupiwa yeye. Hili ndilo soka la Tanzania ambalo binafsi naona kuna wakati linatia kichefuchefu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -