Friday, December 4, 2020

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA JEREMIA ERNEST

JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa mwambao aliendelea kutumia jina hilo hilo ambapo mpaka leo limebaki kwenye kumbukumbu za mashabiki.

Hata kama sura yake imekupotea unaweza kuingia katika mtandao YouTube na kutafuta nyimbo zake maarufu kama Utalijua Jiji, Una Jidodo Limekuganda, Ngoma Iko Huku na Hamniwezi utagundua ukubwa wake kwenye muziki wa taarabu.

AFUA NI NANI?

Miaka kadhaa iliyopita katika mitaa ya Temeke Veteran, Afua a.k.a B 52, alizaliwa na akapata nafasi ya kusoma shule ya msingi, Temeke.

Afua ambaye ameolewa  na mama wa watoto wanne na wajukuu wanne, hakuweza kujiunga na elimu ya sekondari kwa sababu alipata mchumba.

HARUSI YA MTOTO YAMPA SHAVU

Akizungumza na safu hii, anasema aliingia kwenye sanaa  kupitia harusi ya mtoto wa marehemu dada yake.

Anasema alikuwa anapenda kuimba ila hakuwahi kupata nafasi mpaka walipokodi bendi ya Ijibushe Taarabu Band kutumbwiza.

 “Niliwafata viongozi wa bendi kuomba nafasi wakaniita kwenye mazoezi siku ya kwanza, niliimba wimbo wa Tupendane wenye maudhui ya kihindi.

“Baada ya kuimba waliona naweza nikaanza kufanya nao kazi ambapo nilirekodi nyimbo ya Pendoni katika studio za radio ya Taifa,” anasema Afua.

Anasema  kwa kuwa muziki kuwa bado hauna nguvu, nyimbo hiyo haikutamba ila wengi walikuwa wakiitumia kwenye shughuli mbalimbali japo hawakufahamu mwimbaji ni yeye.

ALIVYOPATA USTAA

Baada ya kumaliza mkataba, alijiunga na bendi ya Melody iliyokuwa na makao makuu Magomeni Kagera kipindi hicho, akapewa nyimbo nyingi hivyo akaanza kupata mashabiki wanaomfatilia kutokana na bendi hiyo ni kubwa na ilikuwa na shoo za mara kwa mara.

Baada ya muda akapewa wimbo, Utalijua Jiji ambayo ilimfanya awe maarufu zaidi ndani na nje ya Tanzania.

“Utalijua Jiji ndio nyimbo iliyonipatia umaarufu na ustaa ukapamba moto kwa sababu wimbo huo ulipendwa na watu wa rika  na jinsia zote,” anasema Afua.

VIPI KUHUSU MAFANIKIO, CHANGAMOTO?

“Kitu pekee ambacho naweza kujivunia kwa sasa kwenye sanaa ni kujulikana na watu tofauti pia kupata msaada unaolingana na hadhi yangu ninapofikwa na matatizo.

 “Changamoto ni kwamba wakati naanza, pesa haikuwepo hivyo ilinibidi kuwekeza ili kuja kupata mafanikio,” anasema.

Aliongeza kuwa hapendi kuongelea changamoto nyingi kwa sababu atawahusisha watu waliotangua mbele za haki ambayo haipendezi kwenye jamii.

MBONA HASOMEKI SIKU HIZI?

Akizungumzia kuhusu kupotea kwake kwenye sanaa, mkataba alioingia na bendi ya Melody uliisha hakuweza kuongeza tena.

“Tulikuwa tunapewa mikataba kwenye bendi wangu ulipoisha sikuweza kusaini tena hivyo sikuwa na bendi japo siku moja moja naenda kupiga ndondo wakinihitaji,”anasema.

Anasema sasa hivi vikundi vimekuwa vingi ila pia umri umeenda ndio maana anawaachia wengine wafanya muziki.

 “Sasa hivi nikifanya muziki nafanya kwa kujifurahisha tu kwa sababu umri umeenda sifanyi, mashindano kama ilivyokuwa zamani,” anasema Afua.

ASHANGAA WAIMBAJI WA SASA

Anasema muziki bado upo una mashabiki wengi tatizo wasanii wa sasa sio wabunifu.

“Wasanii sasa hivi wanaimba kopi zaidi kuliko kutafuta nyimbo zao, wasijue kuwa wakiimba ngoma ya mtu wanazidi kumpa ujiko,” anasema.

Aliongeza kuwa wapambane kutengeneza vyao ili kujenga majina yao ambapo watapata faida zaidi wasiridhike na wanachokipata kupita ngoma za watu.

Anasema mfano mzuri wa kuigwa kwa wasanii wa sasa ni Isha Ramadhani ‘Isha Mashauzi’ alipambana akajipatia jina sasa analia kivulini.

SABABU ZA KUWA KIMYA

Katika mahojiano yake na safu hii, anasema anaishi Jangwani jijini Dar es salaam akifanya biashara ndogo ndogo.

Anasema kwa sasa hana nyimbo ambayo ipo tayari ila ikitokea akapewa anaimba kama kawaida kwa sababu ng’ombe hazeeki maini.

“Bado napenda muziki wa taarabu nikipewa nyimbo nitaifanyia kazi na itatoka poa sauti bado ninayo, mara nyingi naitwa kwenye bendi ya Gusa gusa inayopiga kila wikiendi ambapo huwa naimba kidogo,” anasema Afua.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -