Sunday, January 17, 2021

Aggrey Morris umeanza kutumia kinywaji gani kaka?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

AGGREY Ambros Morris, mara ya mwisho tulipokutana na kuzungumza kule Chamazi, kama sikosei miaka mitatu iliyopita, ulinihakikishia kuwa hutumii vinywaji vingine zaidi ya maji, maziwa na juice.

Nilibisha? Hapana, uso wako, sauti yako na tabia yako ndani na nje ya uwanja vilionyesha kuwa ni mtu uliyebobea na vinywaji hivyo tu. Maji yalikupa nuru, juice ikikupa afya, namkumbuka sana Aggrey yule!

Nahodha aliyeiongoza Azam kubeba ubingwa wa ligi bila kufungwa mchezo wowote, beki aliyekuwa kwenye mioyo ya Watanzania wakikupigia chapuo la kurithi moja na nafasi mbili kwenye kikosi cha Taifa Stars, kama si Kelvin Yondani basi Nadir Haroub ‘Cannavaro’, mmoja wao alitakiwa kukupisha. Unazikumbuka zile nyakati?

Mpaka leo sielewi kwanini ulipokonywa unahodha, sielewi kwanini haumo tena kwenye midomo ya Watanzania, lakini kibaya zaidi sielewi ulikoutoa moyo ulioubeba ndani yako kipindi hiki, umeacha kutumia vile vinywaji?

Matukio mengi ya kutisha kwa wachezaji yamekuwa yakitoka kwako, ni wewe uliyemzimisha Emmanuel Okwi, ni wewe uliyempa jeraha zito Abasirim Chidiebere na ni wewe uliyekaribia kumfanyia tukio la ajabu Obrey Chirwa, nini kimebadilika kaka?

Tunaweza kusema ni matukio ya mchezo, ndio maana hakuna aliyekushutumu mpaka leo, lakini kwanini ni wewe kila siku? Nafsi yako haioni aibu kwa matukio haya?

Aggrey yule aliyekuwa kiongozi wa amani kwa wengine ndio amekuwa kiongozi wa matukio yasio ya kiungwana kwa wengine, nini wajifunze kina Sure Boy na Himid Mao?

Hawa vijana kama Andrew Vicent wanatakiwa wafuate njia kutoka kwao, hebu rudi na umtazame kwa makini rafiki yako Nadir Haroub ‘Cannavaro’, mpaka wakati huu akielekea mwisho wa safari yake, amebaki kuwa beki anayeheshimika na mfano wa kuigwa kwa wengine.

Kwanini umewaangusha Watanzania? Wengi waliokuwa na imani kubwa na wewe wameanza kuogopa kusema jina lako hadharani, uungwana wako unakwenda wapi?

Nilishindwa kujibu watu moja kwa moja kabla sijapata jibu lingine kutoka kwako, umeanza kutumia kinywani gani kinachokujaza ari na hasira namna hiyo?

Ni kinywaji hicho kinachokufanya usahau uungwana wako ukiwa uwanjani? Kama bado ni maji na juice, nijuze ili tuanze upelelezi wa nini kinachanganywa ndani yake. Bado nakuhesabu kama beki bora nchini, unapopita sipo, rudi na uanze upya!

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -