Thursday, December 3, 2020

AHMAD AANZA KUIBUA ‘UCHAFU’ WA HAYATOU CAF

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

CAIRO, Misri

RAIS wa Shirikisho la Soka barani Afrika (Caf), Ahmad Ahmad, haonekani kuridhishwa na ‘madudu’ ya mtangulizi wake, Issa Hayatou na tayari ameshaanza kuyaibua.

Wakati wa kampeni kabla ya kuingia madarakani mwezi uliopita, alitamka wazi kuwa utawala wa Hayatou ulikuwa wa kifisadi, hivyo anataka ‘kuifufua’ Caf iliyokuwa imeuliwa na Mcameroon huyo.

Hivi karibuni alitangaza kuwa ataanza kupitia nyaraka zote za haki za matangazo ya runinga katika fainali za Mataifa Afrika za mwaka huu (Afcon 2017).

Ahmad alipinga mkataba wa muda mrefu wa miaka 12 wa kurusha matangazo kati ya Caf na kituo cha televisheni cha Lagardere Sports cha Ufaransa.

Lakini pia, alihoji uhalali wa mchakato wa kuipa Lagardere haki ya kurusha michuano yote inayoandaliwa na Shirikisho hilo, akisisitiza kuwa kulikuwa na harufu ya rushwa wakati wa ugawaji wa tenda hiyo.

“Tutachunguza lakini bado nina wasiwasi na urefu wa mkataba huo. Sitasaini mkataba wa zaidi ya miaka mitatu.

Aidha, Ahmad amesema anaangalia uwezekano wa kuifanyia marekebisho makubwa michuano ya Afcon ili iweze kutoa nafasi kuwa wachezaji wanaocheza Ulaya.

Wachezaji wengi wa Afrika wanaocheza barani humo hushindwa kuja Afcon kwani wakati wa michuano hiyo klabu zao huwa katikati ya msimu.

Katika fainali za mwaka huu za Gaon, wachezaji tisa wa Cameroon walishindwa kujiunga na timu hiyo kwa kuwa klabu zao Ulaya zilikuwa zikiwahitaji.

“Ni wachezaji wakubwa ndio wanaoyafanya mashindano yanoge. Nitazungumza nao na kuona ni jinsi gani wanavyojisikia kuhusu michuano hiyo,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -