Tuesday, October 20, 2020

AJIB AELEZA KILICHOMCHELEWESHA MORO

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

 SAADA SALIM NA MARTIN MAZUGWA


 

NYOTA wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajib, ameondoa hofu kwa Wanajangwani juu yake na kusema kwamba, kilichosababisha ashindwe kwenda Morogoro ni kutokana na kuumwa malaria.

Awali, Ajib alishaanza mazoezi na wachezaji wenzake jijini Dar es Salaam, pia alianzia benchi katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) dhidi ya Gor Mahia, lakini wiki chache zilizopita Ajib alishindwa kuungana na Yanga iliyopo Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao mwingine wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.

Yanga imetinga mkoani humo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Agosti 19, Uwanja wa Taifa, pia kwa lengo la kujifua na mtanange wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.

Akizungumza na BINGWA jijini jana, Ajib alisema amechelewa kuungana na wenzake katika kambi hiyo kutokana na kuumwa malaria, hali iliyomfanya kushindwa kwenda.

“Niko Dar es Salaam, naumwa malaria ndio sababu sijaenda Morogoro, nitakapojisikia vizuri nitaenda kambini kujiunga na wenzangu kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu ujao,” alisema.

Ajib alisema tayari ameshaanza matibabu na kutumia dawa, muda wowote kuanzia leo akijisikia vizuri ataungana na wenzake katika kambi hiyo ya Morogoro.

Wakati huohuo kiungo wa Yanga, Mohamed Issa ‘Mo Banka’, amesema anatarajia kuungana na timu itakaporejea Dar es Salaam kwani hivi sasa amerudi visiwani Zanzibar, kumuuguza mkewe.

Mo Banka amesajiliwa msimu huu na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Mtibwa Sugar.

Akizungumza na BINGWA jana kutoka visiwani Zanzibar, Issa alisema ameshindwa kuungana na timu Morogoro, kutokana na kuuguliwa na mkewe, alipata taarifa za kuumwa kwake alipokuwa na timu jijini Dar es Salaam.

“Nafurahi hivi sasa hali ya mke wangu inaendelea vizuri, natarajia kuungana na timu wiki hii baada ya kurejea kutoka Morogoro,” alisema.

Katika hatua nyingine, Banka alisema kuwa licha ya kufanya mazoezi kwa siku tatu na Yanga, anaamini atarejea katika kiwango chake hii ni baada ya kukaa nje kwa kipindi kirefu akisumbuliwa na majeraha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -