Friday, October 30, 2020

AJIB AIBUA MJADALA NYETI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

|  HUSSEIN OMAR NA MWAMVITA MTANDA    |          

ACHANA na pointi tatu alizoipa timu yake dhidi ya Mbao FC kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, pasi iliyozaa bao la kwanza kutoka kwa Ibrahim Ajib, vimeibua mjadala mpya ndani ya Yanga.

Juzi usiku, kwa mara nyingine Ajib aliibuka kuwa shujaa wa Yanga baada ya kuiwezesha kubeba pointi zote tatu katika mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kuifanya timu hiyo kufikisha pointi 16 kutokana na mechi sita.

Katika mchezo huo ulioanza saa 1:00 jioni na Yanga kupata ushindi wa mabao 2-0, Ajib ndiye aliyepika bao la kwanza lililofungwa na Rafael Daudi baada ya mpira wake wa adhabu kutoka wingi ya kulia kutua kichwani kwa mfungaji huyo na kuutumbukiza nyavuni.

Dakika ya 90, Ajib alijithibitisha kama mmoja wa wachezaji tishio hapa nchini, akiwa na kipaji cha kipekee baada ya kufunga bao ‘bab kubwa’ lililoihakikishia Yanga ushindi.

Akiwa nje kidogo ya 18, Ajib aliuona mpira uliookolewa na mmoja wa mabeki wa Mbao ukimfuata eneo alilokuwapo na kuupiga kwa mtindo wa ‘tiki taka’, uliompa umaarufu mkali wa Ghana, Anthony Yeboah na mpira kujaa nyavuni.

Kabla ya kutwaa nyavuni, mpira huo uligonga mwamba wa juu na kuipatia Yanga bao la pili.

Saa chache baada ya bao hilo, kocha mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, aliliambia BINGWA kuwa atampa nafasi Ajib katika mchezo wa kikosi chake hicho dhidi ya Lesotho wa kuwania tiketi ya fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon 2019), zitakazopigwa mwakani nchini Cameroon.

Amunike alisema japo hakwenda Uwanja wa Taifa lakini aliushuhudia mchezo huo kupitia runinga na kuvutiwa mno na kiwango cha Ajib, zaidi likiwa ni bao lake hilo.

“Katika mechi zote ambazo nimemwangalia (Ajib), nimegundua ni mchezaji mzuri, ana kiwango cha kimataifa, ninamuhitaji sana katika kikosi changu, lakini katika mechi hii ijayo (dhidi ya Cape Verde Oktoba 12, mwaka huu), amechelewa, nitampa nafasi mechi ijayo dhidi ya Lesotho,” alisema Amunike.

Juu ya bao alilofunga Ajib, nyota huyo wa zamani wa Nigeria alisema: “Kwa staili ya bao alilofunga jana ni wachezaji wachache Afrika wenye ufundi wa aina ile ya ufungaji.”

Kwa upande wa watu wa Yanga, bao la Ajib na kiwango chake na timu yao kwa ujumla, vimezua mjadala nyeti mno ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.

Mjadala huo si mwingine bali ni ule unaoonekana kupigwa chenga kwa muda mrefu, yaani Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo ambao hadi sasa haujajulikana utafanyika lini.

Mara baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Mbao, mashabiki wa Yanga waliokuwa nje ya Uwanja wa Taifa, walikuwa wakilalamikia kitendo cha Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuwa kimya kuhusiana na suala zima la uchaguzi wa viongozi baada ya mabosi wao kujiuzulu.

“Hebu fikiria timu inacheza hivi wakati haina uongozi wowote wa maana, nadhani inabidi tushinikize uchaguzi ufanyike ili tupate viongozi watakaozidi kuwapa morali wachezaji la sivyo tutapotea,” alisema mmoja wa mashabiki wa timu hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Khatibu wa Keko Machungwa, huku akiungwa mkono na wenzake.

Kwa upande wake, mmoja wa wanachama maarufu wa Yanga, Abbas Tarimba, alisema timu yao ni nzuri lakini inakosa morali kutokana na matajiri wengi kukaa pembeni kutokana na viongozi waliopo sasa klabuni hapo.

“Timu iko vizuri, lakini ndio hivyo, sisi wengine hatuna maneno mengi zaidi ya vitendo, lakini kama uchaguzi unafanyika na viongozi wanapatikana, itakuwa nzuri zaidi, ’’ alisema Tarimba.

Naye mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Tobias Lingarangala, alisema suala la uchaguzi haliwezi kuepukika ndani ya klabu hiyo.

“Suala la uchaguzi haliepukiki, tunaomba watu wenye dhamana ya kuandaa uchaguzi wafanye haraka kwani siku zinakimbia, timu haina uongozi wa maana,’’ alisema Lingarangala.

Tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, klabu hiyo imekuwa ikiendeshwa chini ya usimamizi wa wajumbe wa kamati za usajili na mashindano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -