Monday, August 10, 2020

Ajib apiga mbili, Simba ikiichapa Lyon 5-0

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MWANDISHI WETU

KIKOSI cha Simba, jana kiliifanyia maangamizi timu ya African Lyon inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza baada ya kuichapa mabao 5-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kipigo hicho cha ‘mbwa mwizi’ ambacho Wekundu wa Msimbazi hao walikitoa asubuhi, kilichangiwa na mabao mawili yaliyofungwa na nyota wa Simba, Ibrahim Ajib.

Ajib alifunga mabao hayo katika dakika ya 25 na 30, huku mengine yakiwekwa nyavuni na Tairone Dos Santos dakika ya 28, Muzamiru Yassin dakika ya 32 na Deo Kanda aliyetokea benchi akikamilisha kalamu hiyo ya mabao dakika ya 87.

Katika mchezo huo, Kocha wa Simba, Sven Vandenbroeck, aliwapanga wachezaji ambao hakuwatumia kwa asilimia 100 katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC ambao Wekundu wa Msimbazi hao walishinda mabao 3-0.

Wachezaji waliopata nafasi ya kuanza jana asubuhi ni kipa Ally Salim, Haruna Shamte, Gadiel Michael, Yusuph Mlipili, Santos, Mzamiru, Francis Kahata, Clatous Chama, Meddie Kagere na Ajib.

Baadaye, kocha huyo aliwaingiza Shiza Kichuya, Kanda, Cyprian Mpenye na Rashid Juma waliochukua nafasi za Kagere, Kahata, Shamte na Mlipili.

Ukiachana na mabao aliyofunga, Ajib alionyesha kiwango cha juu, hivyo kufuata nyayo za kiungo Said Ndemla aliyekinukisha juzi walipovaana na Mwadui.

Kutokana na hali hiyo, nyota wa Simba, Kanda, Kahata, Sharaf Shiboub na wengineo, hawana budi kukaza buti ili kunusu nafasi zao mbele ya mafundi hao wa mpira (Ajib na Ndemla).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -