Sunday, November 29, 2020

AJIB ATOA YA MOYONI SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA


STRAIKA kipenzi cha mashabiki Simba, Ibrahim Ajib, ameibuka mafichoni na kuzungumzia mustakabali wake ndani ya kikosi hicho cha Wekundu wa Msimbazi.

Ajib ambaye kwa siku za karibuni amekuwa akihusishwa na watani wao wa jadi, Yanga, mkataba wake unamalizika kati ya Desemba mwaka huu.

Akizungumzia mustakabali wake ndani ya kikosi hicho cha Simba ambacho kimeanza mazoezi kwa ajili ya mzunguko wa pili, Ajib alisema mpaka sasa yeye bado ni mchezaji halali wa Simba.

“Kwani nimemaliza mkataba Simba? Sasa kama sijamaliza kwanini watu wanizungumzia kila kukicha? Mimi bado nina mkataba,” alisema.

Alipoulizwa kwanini anagoma kusaini mkataba mpya na tetesi za kuhamia Yanga, Ajib alicheka na kusema: “Hizo taarifa kwangu ni mpya na ndiyo kwanza nimeanza kuzisikia sasa.

“Mimi ndio nakusikia wewe unasema hayo maneno kwa kweli wala sijui chochote kile kinachoendelea,” alisema.

Alipotakiwa kufunguka zaidi, Ajib alihoji: “Hivi kwanini Ajib, mbona awamzungumzii wachezaji wengine? “Alafu nikwambie tu vitu vingine mnavyosema wala si kweli, mfano eti Said Ndemla anakaribia kumaliza mkataba, nani kawaambia yule anamaliza mwakani wala si sasa kabisa kama mnavyosema.”

BINGWA halikuchoka likamtaka Ajib kutoa kauli yake kwa mashabiki wake wa Simba na straika huyo kipenzi cha mashabiki alisema: “Unataka kunitega sasa? Mimi nawaambia nini mashabiki? Huu unanipa mtihani wallah,” alisema.

Kuhusu suala la lini atakaa na vigogo hao wa Simba kuongeza mkataba mpya, Ajib aliomba akate simu na kuahidi kupiga baada ya dakika tano kwa ajili ya kuendelea na mazungumzo.

“Naomba nikupigie baada ya dakika tano kuna kitu kidogo nafanya nikimaliza nitakupigia, nakuahidi nitakupigia mwenyewe wala usijali,” alisema.

Lakini muda ulivyozidi kwenda alipotafutwa simu yake ilikuwa ikiita bila majibu yoyote na mpaka tunakwenda mitamboni ilikuwa haipokelewi.

Ajib na nyota wengine ambao wanamaliza mikataba yao kwenye kikosi hicho nahodha Jonas Mkude na kiungo Said Ndemla, wamekuwa wakiwapa presha mashabiki na vigogo wa timu hiyo.

Nyota hao wanatarajia kumaliza mikataba yao kati ya Desemba, mwaka huu na Juni, mwakani.

Nyota wengine ambao wako mwaka wa mwisho wa mikataba yao ni Ajib, kipa Vincent Angban, mabeki Jjuuko Murushid na kiungo Mwinyi Kazimoto.

Kwa jinsi walivyoitumikia Simba mzunguko wa kwanza, wachezaji wote hao ni muhimu mno katika kikosi cha Wekundu wa Msimbazi hao kiasi kwamba iwapo wataondoka bila shaka watakuwa wamewaliza mashabiki wengi wa timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -