Thursday, October 22, 2020

AJIB ATUA MORO KUNOGESHA KAMBI

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

NA MICHAEL MAURUS, MOROGORO                 |                        


 

MSHAMBULIAJI wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajib, jana ameripoti kambini mjini hapa na  kuungana na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara, pamoja na mechi zao za kimataifa.

Kikosi cha Yanga kilianza kambi mjini hapa tangu wiki iliyopita, lakini Ajib alikuwa miongoni mwa wachezaji walioshindwa kufanya hivyo na kubaki jijini Dar es Salaam akidaiwa kuugua malaria.

Ajib ametua katika kambi ya timu hiyo iliyopo Heteli ya KingsWay eneo la Msamvu, lakini akiwakuta wenzake wakiwa wameshaiva tayari kuuwasha chini ya kocha mkuu, Mwinyi Zahera.

BINGWA lilimshuhudia Ajib akiwa eneo la hoteli hiyo jana jioni ambapo alikuwa tayari ameukosa mchezo wa kirafiki dhidi ya Morogoro Tanzanite Academy, uliochezwa asubuhi kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia, ambapo Yanga ilishinda mabao 5-1.

Mbali ya Ajib, wachezaji wengine waliochelewa kujiunga na wenzao kambini ni kipa Radhaman Kabwili aliyetua juzi mchana pamoja na Mohamed Issa ‘Mo Banka’.

Kikosi cha Yanga kinajiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu lakini pia mechi yao ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya nchini Rwanda.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -