Monday, October 26, 2020

AJIB KUZIBA NAFASI YA SAMATTA ?

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA TIMA SIKILO

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Ibrahim Ajib, ameahidi kutomwangusha Mbwana Samatta, iwapo atapewa nafasi katika kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, kuchukua nafasi yake.

Samatta ataukosa mchezo ujao wa Stars dhidi ya Lesotho wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon), kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano katika mechi mbili dhidi ya Cape Verde, ugenini na nyumbani.

Kadi ya njano ya pili ya Samatta aliipata juzi wakati Stars ilipoichapa Cape Verde mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku nyota huyo anayekipiga Genk ya Ubelgiji akifunga bao moja na kutoa pasi ya bao, japo alikosa penalti.

Kabla ya Stars kuifuata Cape Verde kwao, Amunike aliweka wazi mpango wake wa kumjumuisha Ajib katika kikosi kitakachoivaa Lesotho akiamini ana uwezo wa kuisaidia timu yake.

Amunike, aliliambia BINGWA: “Nimegundua (Ajib) ni mchezaji mzuri, ana kiwango cha kimataifa, ninamhitaji sana katika kikosi changu, lakini katika mechi zijazo (dhidi ya Cape Verde), amechelewa, nitampa nafasi mechi dhidi ya Lesotho.”

Kwa upande wake, Ajib ameliambia BINGWA jana kuwa yupo tayari kuitumikia Stars muda wowote, hivyo endapo ataitwa kuziba pengo la Samatta, hatamwangusha nyota huyo.

Alisema anafurahishwa na jinsi ambavyo mashabiki wa soka wamekuwa wakimwamini, akiwataka kuendelea kuwa na imani naye, huku akiweka wazi jinsi alivyofurahishwa na ushindi wa Stars dhidi ya Cape Verde juzi.

“Nimefurahi kuona timu yetu haijaruhusu kufungwa nyumbani, kama nitapata nafasi ya kuitwa mchezo ujao basi nitapambana, mashabiki wasijali,” alisema.

Ajib amejizolea sifa kutokana na uwezo wake wa kutoa pasi za mabao, akiwa amechangia mabao matano kati ya 11 ya timu yake ya Yanga katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -