Tuesday, November 24, 2020

AJIB, MAVUGO KUMNG’OA BOSSOU YANGA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

HOMA ya pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, imezidi kupanda kwa pande zote mbili, huku Wekundu wa Msimbazi wakionekana kuwa na matumaini makubwa na washambuliaji wao ‘mapacha’, Ibrahim Ajib na Laudit Mavugo kuwa lazima watawaangamiza watani wao hao na hivyo kuhatarisha kibarua cha beki wao, Mtogo Vincent Bossou.

Mahasimu hao wanatarajiwa kukutana Februari 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka wa maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Katika mechi za hivi karibuni za Simba, Ajib na Mavugo wameonekana kucheza kwa uelewano wa hali ya juu kiasi cha kutengeneza kombinesheni hatari inayowapa jeuri watu wa Simba wakiamini wakali wao hao wanaweza kuwa mwiba mchungu kwa Bossou na wenzake Februari 25.

Mbali ya Bossou, wengine wanaoweza kujikuta katika wakati mgumu kwa Ajib na Mavugo iwapo hawatakuwa makini siku hiyo, ni beki mwenzake wa kati, Kelvin Yondani, Juma Abdul (kulia) na Haji Mwinyi (kushoto).

Utamu wa Ajib na Mavugo unatarajiwa kutiwa ‘chachandu’ na Mohammed Ibrahim ‘Mo’ ambaye naye ameonekana kuwa ni moto wa kuotea mbali kama alivyojidhihirisha katika mechi za hivi karibuni za Simba.

Kwa upande wao, Ajib na Mavugo walidhihirisha kuwa wao si watu wa mchezo mchezo wakati Simba ilipoikaribisha African Lyon katika mchezo wa Kombe la FA uliopigwa juzi Uwanja wa Taifa baada ya kuonyesha viwango vya hali ya juu na kuwafanya mashabiki wao kuwashangilia mno, huku wale wa Yanga wakibaki midomo wazi.

Kutokana na uchezaji wao, wamekuwa wakitengenezeana nafasi za kufunga kiasi kwamba akikukosa Ajib, utafungwa na Mavugo.

Tayari Mavugo ametamba kukinukisha Februari 25, watakapowavaa Yanga akitamba kuwa kwa jinsi anavyoelewana na Ajib, hadhani kama kuna beki wa kuwazuia wa watani wao hao wa jadi.

“Hatuna mengi ya kuzungumza zaidi ya kupambana kuhakikisha tunafurahisha mashabiki wetu ambao wana hamu kubwa ya kuona timu yao ikitwaa ubingwa msimu huu,” alisema.

Lakini ikumbukwe kuwa kwa mara kadhaa Bossou amekuwa akitamba kuwa hakuna mshambuliaji wa Simba anayemsumbua akitolea mfano jinsi alivyomdhibiti Mavugo na kujikuta akitolewa katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi.

Simba imeondoka Dar es Salaam kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo huo ambao unatabiriwa kuwa na upinzani wa hali ya juu kutokana na ubora wa timu zote mbili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -