Sunday, November 29, 2020

Akilimali akubali ‘mabadiliko’ Yanga

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

KATIBU wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Akilimali akubali ‘mabadiliko’ Yanga, ameupongeza mpango wa uongozi wa timu hiyo kutaka kumleta kocha wa timu za ZESCO United ya Zambia, Mzambia George Lwandamina, ili kukinoa kikosi hicho.

Yanga imekuwa ikihusishwa na mipango ya kufikiria uamuzi wa kumchukua kocha huyo, baada ya kuona timu yao ikiwa imeshuka kiwango na hivyo kuhofia huenda wakashindwa kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Hivi karibuni baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 dhidi ya watani zao Simba, uongozi wa Wanajangwani hao ulikutana na kutathmini juu ya mwenendo mzima wa kikosi chao, lakini pia wakiyarejea matokeo ya kufungwa 1-0 na Stand United mjini Shinyanga.

Akizungumza na BINGWA, Akilimali alisema moja kati ya mambo muhimu yaliyofanywa na uongozi wa sasa chini ya bilionea wa timu hiyo ni juu ya mpango wa kumleta kocha huyo.

“Tumepokea kwa furaha sana hizi taarifa za kutaka kumleta huyu kocha Lwandamina, sisi kama wazee wa timu tunabariki kwa asilimia mia moja mpango huu,” alisema Akilimali.

Aliongeza kuwa benchi la ufundi la Yanga linahitaji marekebisho kutokana na makocha waliopo hivi sasa kuonekana kuzidiwa kimbinu na makocha wa timu nyingine.

“Kusema kweli kocha wetu, Hans van der Pluijm, uwezo wake wa kufundisha umeishia pale tunaweza kusema pumzi imekata, tukubali au tukatae lazima apatikane mtu wa kupokea kijiti chake,” aliongeza Akilimali.

Taarifa ambazo BINGWA imezipata kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, zinasema kocha Lwandamina atakuja nchini Desemba mwaka huu, kuchukua mikoba ya Mdachi, Hans van der Pluijm, ambaye atapewa majukumu ya ukurugenzi wa benchi la ufundi hasa kutokana na mfumo wa mabadiliko unaofanywa na klabu hiyo.

Aidha, taarifa hizo zinasema kutokana na jinsi Pluijm alivyoweza kuiongoza Yanga na kutwaa mataji mawili (Ligi Kuu Bara na Kombe la FA), hawawezi kumfungashia virago na hivyo wameona wampe ukurugenzi ili  aweze kulisaidia benchi la ufundi litakaloongozwa na Lwandamina kuhakikisha ina pata mafanikio katika ligi ya ndani na mashindano ya klabu bingwa mwakani.

Iwapo Pluijm ataondolewa katika nafasi ya ukocha kwa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, atakuwa ni watatu katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita lakini chanzo kikiwa ni matokeo ya mechi dhidi ya Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -