Friday, December 4, 2020

Akilimali atengua kauli Yanga

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA WINFRIDA MTOI,

BAADA ya mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa kuanza kufunga, Katibu wa Baraza la Wazee wa timu hiyo, Ibrahim Akilimali, ametengua kauli yake aliyowahi kutoa juu ya mchezaji huyo na kusema kuwa hana tatizo naye kwa sasa.

Akilimali aliwahi kutoa kauli siku za nyuma kuwa anashangazwa na kitendo cha Yanga kumsajili mchezaji huyo kwa pesa nyingi, wakati ameshindwa kuonyesha kiwango kama ilivyotarajiwa.

Chirwa, aliyesajiliwa na Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, alikuwa na wakati mgumu ndani ya  timu hiyo kutokana na kutokubalika kwa mashabiki, hasa kwa kushindwa kuonyesha ubora wake uliomfanya kununuliwa kwa pesa nyingi.

Mshambuliaji huyo hivi sasa ameonekana kama anaanza kuwaumbua wale waliotoa kauli mbovu juu yake ambapo katika mechi za hivi karibuni ameanza kuonyesha uwezo wa kufunga.

Tangu ametua nchini, bao lake la kwanza alifunga kwenye mechi ya Ligi ya Vodacom Tanzania Bara na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, akafunga  bao la pili katika mchezo  na Toto African kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Hiyo haitoshi, mwishoni mwa wiki alitupia mabao mawili kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera, wakati Yanga ilipoibuka na ushindi mnono wa mabao 6-2 na kufikisha idadi ya mabao manne katika msimamo wa wafungaji wa ligi.

Akizungumza na BINGWA jana, Akilimali alisema kwa sasa anamuunga mkono Chirwa na awali alitoa kauli hiyo baada ya kuona hafanyi vizuri katika mechi za kimataifa ambazo ndio lengo la kusajiliwa kwake.

“Chirwa ni mchezaji wetu, ameanza kuonyesha uwezo, naomba mashabiki wa Yanga tuungane naye na umoja wetu ndio unakaofanya timu yetu kusonga mbele,” alisema.

Alifafanua kuwa, alichokisema haikuwa kumkandamiza Chirwa, bali ilikuwa kama kumuonya mtu aliyekosea baada ya kucheza michezo yote ya kimataifa bila kufunga bao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -