Wednesday, October 28, 2020

ALAN SHEARER AMMWAGIA SIFA AGUERO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

   LONDON, England 


 

NYOTA wa zamani, Alan Shearer, amemmwagia sifa straika wa Manchester City, Sergio Aguero, akisema kuwa ndiye mchezaji bora wa kigeni kununuliwa katika historia ya Ligi Kuu England.

Mpaka sasa hakuna mchezaji yeyote ambaye ameshaweza kufunga mabao zaidi ya 260 ambayo aliyafunga Shearer katika michuano hiyo, lakini staa huyo wa zamani anasema kuwa kwa sasa Aguero ndiye tishio ukiachana na nyota wa zamani Arsenal, Thierry Henry.

Tangu ajiunge na Manchester City akitokea Atletico Madrid mwaka 2011, Aguero, ameshazifumania nyavu mara  146.

Mabao matatu aliyoyafunga katika ushindi wa 6-1 dhidi ya Huddersfield, ilishuhudiwa yakimfanya Aguero kuingia kwenye orodha ya kushindania nafasi ya mfungaji bora wa muda wote akimpiku nyota wa zamani wa  Arsenal na Manchester United, Robin van Persie.

Kutokana na hali hiyo, akizungumza juzi, Shearer alisema kwamba, anavyoamini  Aguero anatakiwa kupewa sifa ya kuwa mchezaji bora wa kigeni na si Henry, Eric Cantona na Cristiano Ronaldo.

“Atatisha tena,” nyota huyo wa zamani wa timu za Newcastle United na  Blackburn Rovers, alisema wakati akichagua timu ya wiki katika michuano ya Ligi Kuu England.

“Kwa sasa ameshafikia hat trick tisa, idadi ambayo inamfanya awe nyuma yangu kwa mbili,” aliongeza staa huyo wa zamani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -