Friday, December 4, 2020

Alba atemwa kikosi cha Hispania

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

SHKODER, Albania

BEKI wa timu ya Taifa ya Hispania, Jordi Alba, ameachwa kwenye kikosi cha timu hiyo ambacho kesho kitaivaa  Albania katika mechi ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia, baada ya kuumia misuli ya nyama za paja katika mchezo dhidi ya Italia.

Katika mchezo huo wa juzi uliopigwa mjini Turin, beki huyo wa Barcelona alipatiwa matibabu kabla ya kutolewa nje ya uwanja dakika ya 22 ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 na nafasi yake ikachukuliwa na staa wa   Real Madrid, Nacho.

Alba, mwenye umri wa miaka 27, alifanyiwa vipimo jana ili kuangalia ukubwa wa tatizo lake na ndipo ikabainika ana jeraha hilo kwenye paja la mguu wake wa kushoto, hivyo ina maana atarudishwa nyumbani.

Kutokana na hali hiyo, Hispania imelazimika kumuita beki wa kushoto wa  Arsenal, Nacho Monreal, ili aweze kuchukua nafasi ya Alba kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya Albania utakaopigwa mjini Shkoder.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -