Monday, October 26, 2020

ALI KIBA KUANZA KAZI COASTAL UNION

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA ZAITUNI KIBWANA


MSHAMBULIAJI mpya wa klabu ya Coastal Union, Ali Kiba, amejiunga na kambi ya timu hiyo na anatarajiwa kuwa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo, kitakachocheza mchezo wa tatu wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya KMC.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Jumamosi hii saa 10:00 jioni, katika Uwanja wa Mkwakwani, mkoani Tanga.

Akizungumza na BINGWA, Ofisa Habari wa Coastal Union, Hafidhi Kido, alisema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mchezo huo na Kiba ni miongoni wa wachezaji hao.

“Timu inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mkwakwani, mwalimu wetu Juma Mgunda anaendelea na kazi yake ipasavyo, nina imani tutaweza kufanya vema,” alisema.

Kiba, ambaye amejizolea umaarufu mkubwa zaidi akiwa kama mwanamuziki ambaye anafanya vema, alisaini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo.

Mchezaji huyo alikosa mechi mbili za mwanzo kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine. Alikuwa nchini Canada kwa ajili ya ziara ya kimuziki.

Coastal Union kwa sasa ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, ikiwa imekusanya pointi nne baada ya kucheza michezo miwili, kushinda mmoja na sare moja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -