Friday, December 4, 2020

ALLEGRI ASHAURIWA KUHAMISHIA MAJESHI ARSENAL

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

TURIN, Italia

MSHAURI wa kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri, Giovanni Galeone, amemdokeza Muitaliano huyo kuhusu dili la kuinoa Arsenal, akimshauri kuondoka Juve ili aweze kuitengeneza timu imara ndani ya dimba la Emirates.

Jina la Allegri ni moja ya majina ya makocha wanaotajwa kurithi mikoba ya Arsene Wenger, iwapo kocha huyo ataondoka Emirates mwishoni mwa msimu huu, kwani bado hajasaini mkataba mpya wa miaka miwili aliowekewa mezani.

Kwa sasa Wenger yupo kwenye presha kutokana na baadhi ya mashabiki wa kutupwa wa Arsenal kupingana na kauli za kwamba kocha huyo atabaki tena Emirates.

Galeone anaamini Allegri, mwenye umri wa miaka 49, anafiti kwenda kuifundisha Arsenal kutokana na mafanikio aliyoyapata Italia.

“Nimemwambia huu ni wakati wa kuondoka Juve, japokuwa si kazi nyepesi. Naamini anao uwezo wa kufanya vizuri ugenini, hasa England kuliko Hispania.

“Anao uwezo wa kuinoa Arsenal, ambayo ni klabu yenye historia kubwa. Naamini anao uwezo wa kutengeneza kikosi imara kwa kuendeleza tamaduni ya soka la Arsenal na wachezaji watazoea haraka mbinu zake. Allegri kwenda Arsenal ni kama ‘zawadi kutoka kwa Mungu’,” alisema mshauri huyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -