Monday, August 10, 2020

Ambokile kuigomea TP Mazembe

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA ZAINAB IDDY

MSHAMBULIAJI wa Kitanzania anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe ya DR. Congo, Eliud Ambokile, ameweka wazi kuwa hayupo tayari kuona anatolewa kwa mkopo katika timu za Tanzania, hivyo ni bora aendelee kukomaa huko huko.

Kauli hiyo ya Ambokile imekuja baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa Mazembe wana mpango wa kumtoa kwa mkopo pamoja na kiungo Ramadhani Singano, katika dirisha lijalo la usajili.

Ambokile alijiunga na TP Mazembe akitokea Mbeya City, huku Singano akijiunga na wababe hao baada ya kuachana na Azam FC, lakini wote hao wamekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.

Akizungumza na BINGWA jana kutoka DR Congo, Ambokile alisema kuwa taarifa za kutolewa kwa mkopo zipo kutokana na ufinyu wa nafasi ya kucheza, lakini bado haijapitishwa kwa sababu viongozi wa timu wanatofautiana.

“Bado haijapitishwa kwa sababu viongozi wanatofautiana katika suala hilo, lakini kama ikipita, sipo tayari kutolewa kwa mkopo katika timu za Bongo (Tanzania), nasubiri wakinipa tu taarifa rasmi, nami nitawaeleza msimamo wangu.

“Natamani sana kupata timu nje ya Tanzania kwa sababu ikitokea nikarudi nyumbani, itakuwa vigumu kuwa kwenye kiwango bora kwa haraka, ni bora nikakomaa katika timu za huku huku au nchi nyingine nje ya Tanzania,” alisema.

Ambokile alijiunga na Mazembe kwa mkataba wa miaka mitatu na tayari ameshaitumikia msimu mmoja na kusaliwa na miwili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -