Wednesday, October 28, 2020

AMMY NINJE MKURUGENZI MPYA WA UFUNDI TFF

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemteua aliyekuwa kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Ammy Ninje, kuwa Mkurugenzi wa ufundi wa shirikisho hilo.

Awali, nafasi hiyo ilikuwa chini ya kocha wa timu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Oscar Milambo, aliyekuwa anakaimu baada ya Salum Madadi kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mashindano.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa wa Habari wa TFF, Cliford Ndimbo, alisema uteuzi wa Ninje umethibitishwa na kamati hiyo katika kikao kilichofanyika Oktoba 20, mwaka huu.

Ndimbo alisema mbali na uteuzi wa Ninje, kamati hiyo ilifanya mabadiliko ya uongozi kwa baadhi ya kamati za TFF na kupitisha tarehe ya mkutano mkuu ambapo utafanyika Desemba 19, mwaka huu jijini Arusha.

Alizitaja kamati zilizofanyiwa mabadiliko kuwa ni Kamati ya Nidhamu ambayo mwenyekiti wake atakuwa Kiomoni Kibamba, Makamu Peter Hella na wajumbe ni Kassim Dau, Handley Matwenga na Twaha Mtengera.

Kamati ya uchaguzi, Mwenyekiti ni Malangwe Ally, Makamu Mwenyekiti ni Mohamed Mchengela na wajumbe ni Benjamini Karume, Mohamed Gombati na Hamisi Zayumba.

Nyingine ni Kamati ya Rufaa na Maadili  ambapo Mwenyekiti wake atakuwa Richard Mbaruku, Makamu ni Thadeus Karua na wajumbe ni Mussa Zungu, ASP Bebedict  Nyagabona na Lugano Hosea.

Kamati ya Tiba, Mwenyekiti atakuwa Dk. Paul Marealle, Makamu ni Dk. Fred Limbanga na  wajumbe ni Dk. Norman Sabuni, Dk. Lisobina Kisongo, Dk.  Eleizer Ndalama, Dk. Billy Haonga na Dk. Violeth Lupondo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -