Friday, December 4, 2020

Amri adai chake Mbeya City

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ASHA KIGUNDULA

ALIYEKUWA kocha wa timu ya Mbeya City, Amri Said, amesema hana anachosubiri zaidi ya kupewa haki zake baada ya uongozi wa klabu hiyo kuvunja mkataba wake.

Juzi  uongozi wa Mbeya City  ulitangaza kumtimua kocha huyo kutokana na mwenendo wa matokeo mabaya ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA jana, Amri alisema viongozi wake ndio waliomuondoa hivyo ana haki ya kupata anachostahili kwa kuwa aliwafanyia kazi.

Amri alisema juzi alikutana na viongozi wa klabu hiyo na kutaka maelezo kutokana na mwenendo wa timu yao na nini anatakiwa kifanyike ili timu iweze kufanya vizuri.

Kocha huyo alisema anashangaa kusikia mkataba wake umevunjwa, kitu ambacho hafahamu na anachohitaji watimize kile walichokubaliana  katika majukumu yake.

Kwa sasa Mbeya City ipo chini ya kocha msaidizi Mathias Wandiba,  ambaye ataendelea kuwa msimamizi wa timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -