Sunday, October 25, 2020

AMRI SAID AITEGA SIMBA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA JESSCA NANGAWE

WAKATI klabu ya Simba ikiendelea kusaka kocha msaidizi ambaye atakuwa mrithi wa Masoud Djuma, kocha wa Mbao FC, Amri Said, ameonekana kuwatega akidai ana uwezo mkubwa wa kuvaa viatu vya Mrundi huyo.

Amri na Selemani Matola ndio wanatajwa kupewa nafasi kubwa na klabu hiyo ya Msimbazi mara baada ya kumalizana na Masoud ambaye ameondoka.

Akizungumza na BINGWA, Amri alisema anaifahamu Simba kila idara lakini jukumu la kupewa nafasi hiyo anauachia uongozi kwa kuwa anaamini ndio wenye kauli ya mwisho.

“Simba wananijua na mimi naijua vyema, jukumu la kupewa nafasi nadhani wanalo wao na kama wananihitaji ni makubaliano tu, haya ni mazungumzo ya awali lakini kila kitu kitawekwa wazi kama tutamalizana,” alisema Amri.

Hata hivyo, uongozi wa Simba ulidai kuwa hauwezi kuweka wazi suala hilo kwa sasa kutokana na mfadhili wao, Mohamed Dewji ‘Mo’, kutekwa na watu wasiojulikana na kuleta hali ya sintofahamu, hivyo kusisitiza kwamba  subira inahitajika kabla ya kutoa uamuzi.

Simba ilimtimua kocha Masoud kutokana na madai ya kuwa katika mgogoro na benchi la ufundi na kuahidi kuleta mrithi wake wakati wowote.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -