Wednesday, October 21, 2020

AMUNIKE ATAMBA KURUDI NA USHINDI STARS

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA SALMA MPELI


KOCHA mkuu wa timu ya Taifa Stars, Emmanuel Amunike, ametamba kurejea na ushindi nyumbani katika mchezo wao dhidi ya Uganda, utakaofanyika keshokutwa nchini Uganda.

Akizungumza na wanahabari jana, Amunike, alisema kikosi chake kipo katika hali nzuri na wanawatambua wapinzani wao, japo utakuwa ni mchezo mgumu lakini imani yake ni kupata matokeo mazuri.

“Ninafurahi kuona kikosi kimekamilika wakiwemo wachezaji wa ndani na wale wanaocheza nje ya nchi, tumejiandaa vizuri na kiufundi tunakwenda kupambana kwa kujilinda na kushambulia pia ili kupata matokeo mazuri na naamini hilo linawezekana,” alisema Amunike.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta, alisema hiyo ni mechi ya majirani kwani timu zote zinajuana na kila mmoja anafahamu uwezo wa mwenzake, kubwa kwao wanajua nini wanatakiwa kufanya na kufikia malengo.

Alisema lengo ni kuhakikisha Tanzania inafanikiwa kucheza Afcon mwakani, hivyo ushindi katika mchezo huo na mechi nyingine zilizopo mbele ni lazima licha ya kutambua kwamba utakuwa ni mchezo mgumu kwa pande zote mbili.

“Tumejiandaa vizuri, hii ni mechi ya majirani kwani sote tunafahamiana, muhimu mimi pamoja na wenzangu tunajua nini tunatakiwa kufanya ili kufikisha timu kwenye michuano ya Afcon,” alisema Samatta.

Kikosi cha wachezaji 23 pamoja na benchi la ufundi la timu hiyo, kinatarajiwa kuondoka leo saa saba mchana kuelekea Kampala, Uganda kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya timu ya The Cranes, kuwania kufuzu mchezo wa Mataifa ya Afrika (Afcon) mwakani.

Uganda watakuwa wenyeji wa mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela, Nambole nchini humo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -