Tuesday, October 27, 2020

AMUNIKE AWAGAWA WADAU WA STARS

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

ZAITUNI KIBWANA, NICE GODFREY (DSJ) DEBORA MBWILO (TUDARCO)


SIKU moja baada ya kocha mkuu wa timu ya Tanzania, Taifa Stars, Emmanuel Amunike, kuwaondoa wachezaji sita wa Simba kwa kosa la kuchelewa kuripoti kambini, uamuzi huo umewagawa wadau wa soka.

Amunike amewagawa wadau hao wa soka baada ya kuwatimua kambini nahodha; John Bocco, Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe pamoja na Hassan Dilunga kutokana na kuchelewa kuripoti kambini.

Kufuatia uamuzi huo, wadau wa soka wamegawanyika huku wengi wakimpongeza na wengine wakipinga uamuzi huo.

BINGWA limezungumza na wadau mbalimbali ambapo mchambuzi, Oscar Oscar, alipinga uamuzi huo kwa kusema kuwa Amunike alipaswa kutumia busara na si kuwafukuza.

“Tunahitaji ushindi au tunahitaji nidhamu? Jibu ni rahisi tu. Tunahitaji ushindi dhidi ya Uganda na tunahitaji wachezaji wetu wawe na nidhamu. Ushindi tunauhitaji kwa haraka, nidhamu inajengwa taratibu. Bado Stars inaweza kushinda bila wao lakini pia inaweza kupoteza kwa kuwakosa wao.

“Kwa kuwaondoa kwenye kikosi ndiyo tutakuwa tumewajengea nidhamu? Akili Yangu inasema hapana. Wanahitaji kupewa uelekeo mpya na mwongozo wa kocha mpya ili waweze kuelewa anachokitaka kocha wao. Kwa sababu hakuwahi kukutana nao, nadhani busara ilihitajika kuwasubiri kwanza na kisha kujua angalau sababu zilizofanya wachelewe kuripoti kambini kabla ya kuwaelekeza utaratibu mpya,” alisema Oscar na kuongeza:

“Hata kama tutashinda dhidi ya Uganda, lakini bado sioni kama tutakuwa tumetatua tatizo la nidhamu kwa wachezaji tuliowaacha.”

Wakati Oscar akiyasema hayo, Ali Kamwe, alimpongeza Amunike kwa kurudisha nidhamu ndani ya kikosi hicho.

“Kwamba tukifungwa na Uganda itakuwa ajabu? Au tusiposhiriki hiyo Afcon itakuwa habari mpya sana? Hakuna kitu. Tufungwe hata 6, 7 au hata 10, ushindi wetu mkubwa tunaotakiwa kujivunia nao kwa sasa ni kitendo cha Amunike kurejesha nidhamu ya jezi ya Taifa Stars,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Ismail Aden Rage, naye amepingana na uamuzi huo kwa kusema kuwa Amunike amewapa adhabu kali wakati wakiwa hawana rekodi ya kufanya hivyo.

“Ni jambo ambalo si sahihi kabisa, nadhani wangeweza kufuatwa na kupewa hata onyo kutokana na kutokuwa na utamaduni wa kuchelewa, au kama ingewezekana wangepigwa hata faini,” alisema.

Nafasi za wachezaji hao zimejazwa na Paul Ngalema wa Lipuli FC, Salumu Kimenya wa Tanzania Prisons, David Mwantika, Frank Domayo wa Azam FC, Salumu Kihimbwa na Kelvin Sabato wa Mtibwa Sugar na Ali Abdulkadir.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -