Sunday, January 17, 2021

Anthony Martial haeleweki duniani, wala mbinguni

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA AYOUB HINJO

MARA nyingi huwa napenda kuwasikiliza wakongwe wakiwa wanazungumzia timu zao za zamani, wakati wote huwa na chembechembe za unafiki fulani hivi usioumiza.

Hawataki kuharibu taswira zao kwa timu na mashabiki, lakini mara zote huwa ‘nainjoi’ zaidi kumsikiliza Roy Keane au Paul Ince wanapoizungumzia Manchester United.

Hawana unafki kama wa Rio Ferdinand au Paul Scholes wa kung’ata na kupuliza, Keane na Ince walivyokuwa uwanjani ndivyo walivyo hata mbele ya televisheni za mashirika ya michezo ambayo mara chache huwaalika kufanya uchambuzi.

Mapema wiki hii, Keane alikuwa anamzungumzia Solskjaer na Manchester United yake, aliichambua kuanzia nyuma mpaka mbele, hakuacha kitu.

Keane imani yake kubwa inamtuma au kuamini bado kikosi cha Solskjaer hakijakamilika, kwanza, inabidi wauze wachezaji ambao hawana msaada kisha wasajili wenye tija na uwezo wa kuisaidia timu hiyo.

Alimzungumzia Marcus Rashford, kisha Jesse Lingard na wengine lakini alipofika kwa Anthony Martial, aliongea maneno mengi zaidi ya aliowazungumzia awali.

Mkongwe huyo aliyekuwa nahodha wa zamani wa Man United, bado hafurahishwi na Martial, macho yake yalimwona mara moja tu akifanya vitu vikubwa baada ya hapo hakumwona tena.

Ni msimu wa Louis van Gaal pekee, Martial aliionyesha dunia miguu yake imebeba vitu vingi ambavyo vilitarajiwa kuonwa na wengi.

Sauti ya Martin Tyler ilisikika kwa mbwembwe ikimkaribisha Martial ndani ya Old Trafford, sauti iliyopenya katika ngoma za masikio za mashabiki wa Manchester United waliojaza vibanda umiza na kumbi za kuangalia mpira. Ilikuwa dhidi ya Liverpool.

‘Ooh! Yeeeees, welcome to Manchester United, Anthony Martiaaaal’. Sauti ya Tyler ilitosha kuwasisimua mashabiki wa Manchester United. Ilitosha kuwakuna moyoni.

Ukweli usiofichika ni kwamba, Martial anaumiza mioyo ya mashabiki wa Manchester United, wanaumia ndani kwa ndani, hawakioni wanachokitaka.

Katika hali hii, nafikiri Anthony Martial angetuhurumia kama Arsene Wenger alivyochagua kuwahurumia mashabiki wa Arsenal.

Kiukweli tunahitaji huruma yake. Vichwa vyetu viko bize sana. Kuendelea kutupa sababu za kumfikiria kila siku ni kutuonea tu.

Binafsi simuelewi Martial, kwanini yuko vile alivyo leo hii. Kwanini hafiki katika picha ambayo mashabiki wa soka wameiweka vichwani kuhusu yeye?

Anaonekana kuwa na kipaji kikubwa sana. Kikubwa mno. Uwezo wake wa kucheza na mpira mguuni ni wa kipekee, wako wachezaji wachache sana wa aina yake.

Siku moja, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema, inahitaji akili ndogo tu kujua kipaji cha Martial kwa kuangalia mkataba waliokubali kuusaini Manchester United kutoka AS Monaco.

Ni wachezaji wangapi unasikia wakisajiliwa kisha katika mkataba wake kukawekwa kipengele cha kutoa hela ya ziada kwa klabu yake ikitokea akashinda Ballon d’Or?

Cristiano Ronaldo hakufanyiwa hivyo. Chelsea hawakukutana na kipengele hiko kwa Eden Hazard. Lakini United walikikuta kwa Martial.

Kwanini? Jibu ni rahisi sana. United walikubali kwa kuwa walitambua thamani na ubora wa Martial katika kipindi kifupi kijacho.

Tazama kilichotokea, Martial alipoteza namba katika kikosi cha kwanza ambacho Jesse Lingard ni panga pangua. Aibu iliyoje hii!

Angalau chini ya Louis van Gaal alianza vyema. Angalau alionyesha kuna kesho inamsumbiri. Lakini, chini ya Jose Mourinho, Martial alikuwa ni mchezaji wa kawaida sana.

Mourinho alimuelezea Martial kama kijana mwenye kipaji kikubwa asiyejituma. Hapa ndipo moyo ya Keane unaumia.

Ni kweli Martial ana kipaji kikubwa. Hili halina punje ya shaka ndani yake, lakini ni kweli hajitumi? Hili ndio swali gumu linalozunguka katika vichwa vyetu.

Kwa kumtazama Martial, kuna upande unaweza kukubaliana na Mourinho halafu kuna upande ukampuuza tu.

Kivipi? Tuanze na upande wa kwanza. Mtazame Kylian Mbappe alivyo kisha rudi kwa Martial. Wote ni vijana lakini unawaona kwenye madaraja mawili tofauti.

Mbappe ni staa tayari. Ameshafanya kazi kubwa katika mechi kubwa. Hana maswali tena. Lakini Martial anaendelea kujikongoja, leo atakufurahisha, kesho atakukera. Haeleweki.

Si kweli kama alikuwa hapati nafasi, hapa tunahitaji kuwa ‘fea’ na Jose Mourinho. Martial alipata nafasi lakini ni kweli uchezaji wake unaonyesha ni mtu anayethamini kwanini amepewa nafasi?

Katika dakika 45 anazoweza kukaa uwanjani, unaweza kumuona katika matukio mawili au matatu. Atapiga mtu chenga ya maudhi, atatengeneza shambulizi, halafu atapotea.

Si mtu anayejituma sana uwanjani. Furaha yake ni kuwa na mpira muda wote mguuni. Wapi tena kuna wachezaji wa aina yake duniani?

Kila kocha anapenda kuwa na mtu mwenye faida nyingi uwanjani na si kushambulia tu. Kuna sababu nyingi za kiufundi zinazomfanya Gabriel Jesus kuwa chaguo la kwanza kwa Pep Guardiola, mbele ya Sergio Aguero.

Mpira wa kisasa unahitaji wachezaji aina ya Roberto Firminho. Sura ya Karrueche Tran, moyo wa Nainggolan. Martial ni mtu wa aina hii? Ni ngumu kumuelezea.

Kwa hali ilivyo, naamini Daniel James atakuwa na pepo nzuri ndani ya Old Trafford kuliko Martial, Solskjaer anamtengeneza James katika nafasi ya Martial.

James hana kipaji kumzidi Martial lakini ana jitihada zaidi ya Martial, kubwa zaidi anaweza kutumika kimbinu kwa ajili ya kuwaumiza wapinzani.

Hili jambo linatuumiza sana wapenzi wa soka. Hatujui ni ukweli upi wa kushika. Je, Martial ni Theo Walcott mpya au ni Mohamed Salah wa baadae?. Maswali ni mengi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -