Tuesday, October 20, 2020

YANGA: KMC TUWACHAPE MANGAPI?

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HUSSEIN OMAR


MABINGWA wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga, leo watashuka katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, kuivaa timu ya KMC ya Kinondoni, huku wakionekana kuwa na matumaini makubwa ya kutoka uwanjani na ushindi.

Na kinachoonekana kwa sasa ndani ya Yanga, ni kama wanachotaka kufahamu ni idadi gani ya mabao wawafunge KMC, kutokana na jinsi wanavyokiamini kikosi chao.

Wanajangwani hao wataingia katika mchezo huo wakiwa na hali ya kujiamini kutokana na mwendelezo mzuri wa kufunga mabao walionao washambuliaji wao wanaoongozwa na Ibrahimu Ajib, Mrisho Ngasa na Heritier Makambo.

Tangu kuanza kwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara, Yanga imeshinda michezo sita na kutoka sare mara moja, katika mitanange saba waliyocheza, hivyo kuufanya mchezo huo wa leo kuwa na mvuto wa aina yake.

Kinachofanya mchezo huo kuwa na mvuto wa aina hiyo ni kutokana na rekodi ya Yanga katika Uwanja wa Taifa, ambao ndio walioutumia kushinda michezo yao yote sita.

Kuelekea mechi hiyo, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, alisema kuwa yeye na vijana wake watahakikisha wanaibuka na ushindi mnono dhidi ya KMC, akiamini kwamba wakati ambao Ligi ni mbichi ndio mzuri zaidi wa kupata matokeo mazuri.

“Najua kwamba ni mchezo mgumu, kwani kila timu inajiandaa ili kushinda, lakini sina presha kabisa na wapinzani wetu. Najua kikosi changu kina uzoefu mkubwa kuliko wao (KMC), malengo yetu ni kuhakikisha tunakusanya pointi tatu kila mchezo,” alisema.

Yanga wanaingia katika mchezo huo wakitoka kutoa dozi ya mabao 3-0 kwa Alliance, mchezo wa Ligi Kuu Bara, uliochezwa Uwanja wa Taifa.

Walinzi wa KMC wakiongozwa na kipa wao, Juma Kaseja, watakuwa na kazi ngumu kuwazuia washambuliaji wa Yanga, hasa Ajib, ambaye amekuwa sumu kubwa kwa timu pinzani kutokana na uwezo wake wa kutengeneza nafasi za mabao.

Ajib amekuwa mpishi mkubwa wa mabao, lakini pia hata yeye mwenyewe amekuwa akifunga kwa staili tofauti tofauti, huku bao lake la ‘tik-tak’ dhidi ya Mbao FC likiwa gumzo mitaani, wengi wakilitabiriwa kuwa bao la msimu.

Wakati mambo yakiwa hivyo kwa Yanga, kwa upande wao KMC kupitia kocha wao, Etiene Ndayiragije, amesema amekiandaa vyema kikosi chake kupambana na Yanga.

Alisema anakiamini vizuri kikosi chake na anategemea watapata matokeo mazuri katika mchezo huo wa leo.

“Nimekuwa nikiifahamu vyema Yanga, kwa kuwa niliwahi kukutana nayo nikiwa kocha wa Mbao na nilikuwa nikipata matokeo mazuri, hivyo naamini haiwezi kunisumbua,” alisema Ndayiragije.

Kuelekea katika mchezo huo wa leo, Yanga itamkosa kiungo wao, Papy Kabamba Tshishimbi, ambaye anasumbuliwa na maumivu ya mguu.

Mratibu wa Yanga, Hafidh aliliambia BINGWA kuwa, Tshishimbi alishindwa kufanya mazoezi na wenzake, hivyo ataukosa mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -