Tuesday, November 24, 2020

ANZA MAISHA UPYA, KATAA MAUMIVU KARIBISHA FURAHA NA AMANI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA RAMADHANI MASENGA,

KUNA jambo kila mtu anatakiwa kuliamua kwa sababu ya amani na furaha ya maisha yake. Kama upo katika uhusiano wa amani na furaha, unatakiwa kuamua kuwa bora zaidi ili amani na furaha yako iweze kuendelea.

Ni vigumu sana kuendelea kufurahishwa na mwenzako ikiwa unafanya matendo ya kumuudhi na kumuumiza. Kuanzia leo, kama unataka kuona amani na raha uliyo nayo katika uhusiano wako inaendelea, kuwa mtu bora na mwafaka katika maisha yake.

Kwa kila kitendo unachotakiwa kufanya hakikisha unakifanya kwa namna inayotakiwa, ila pia kwa kila jambo unalotakiwa kukaa nalo mbali hakikisha unaliepuka ili uweze kumfanya kuwa na amani na utulivu wa nafsi.

Kwa maendeleo ya furaha yako, amua kumpa amani na raha mwenzako. Katika uhusiano, raha huwa ni kitu cha kusababishwa, hasa mkiwa mnapendana. Yaani kama unataka akupe raha na amani, inabidi umsababishe yeye kuwa na amani na furaha. Kiasili, binadamu ana tabia ya kutaka kulipiza kisasi.

Kama ukimfanyia ujinga leo, kuna hatari hata yeye kukufanyia ujinga kesho. Hali hii kwa wengi inaweza isionekane leo au kesho. Wewe kila siku unaweza kumfanyia mwenzako matendo yasiyostahili na ukadhani hajali, ila tambua kuna kitu kitakuja. Siku atakayosema hapana, na kila kitu katika maisha yako kitabadilika.

Kwa mahitaji ya amani yako ya kesho, anza kumpa amani yeye leo. Wengi wenye furaha na amani katika maisha yao ya kimahusiano walianza kutoa amani kwa wenzao kwanza. Walikuwa wapole na wenye maneno mazuri, wakawa bora katika nyanja za kimahusiano na hatimaye wamewafanya wenzao waanze kuwatizama katika namna inayotakiwa.

Huna amani katika uhusiano wako? Kila siku kwako ni ugomvi na karaha, hakuna thamani wala maana ya kuwa katika uhusiano? Umejaribu kila kitu kwa ajili ya kuleta amani katika uhusiano wako umeshindwa? Umekuwa mpole, ukawa mnyenyekevu, ukajifanya pia mjinga ili ajue thamani na hadhi yako katika maisha yake ila ameendelea kuwa tofauti?

Kataa kuendelea kuwa katika uhusiano wa namna hiyo! Kila mmoja anahitajika kuwa na mtu anayempenda na kumheshimu. Amjali na amthamini kwa kiwango cha kipekee na namna iliyo bora.

Mapenzi hayapimwi kwa maneno, ili iwe kweli anakupeda inabidi aoneshe kwa matendo na wakati mwingine kuthibitisha kwa kauli. Sasa kama anakutesa na kila siku anakusababishia maumivu ni kwa namna gani tuseme anakupenda? Kuwa makini. Anza kumsoma mwenzako vizuri. Chunguza  matendo yake kwa kina kuujua ukweli.

Ndiyo, unampenda sana. Huenda akawa ni mtu wa ndoto yako, ila jiulize ni kwa namna gani uhusiano wako utaleta maana kama ukiwa na mtu asiyekupenda? Na kwa namna gani unaweza kupendwa mahali unapoteswa, unadharaulika na kunyanyasika?

Kataa maumivu katika nafsi yako, karibisha furaha na amani. Daima huwezi kuwa na amani kwa mtu asiyekujali wala kuthamini chozi lako. Huwezi kuona raha na furaha ya maisha ikiwa unanyanyasika na kudharaulika.

Ni ngumu kuachana na mtu unayependa, ila pia kuendelea kuishi na mtu unayempenda halafu yeye hakupendi maana yake ni kukubali maumivu na karaha. Kama ulivyokuwa humjui, anza hatua za kumsahau katika maisha yako leo. Kuwa naye, mbali na kukudhoofisha kiakili ila pia anafanya usipate nafasi ya kuwa na mtu atakayekujali na kukuthamini. Yupo wa aina hiyo, achana na mawazo kuwa hakuna kama huyo.

Labda, hakuna atakayekutesa kama huyo ila yupo bora zaidi na mwenye heshima na hadhi zaidi ya huyo. Kubali haya maumivu ya muda mchache ya kuachana naye. Wengi ni waoga kukubali haya maumivu ya muda mchache na matokeo yake wanakuwa na maumivu ya muda wote. Amua kuwa na furaha leo, maisha yako ni yako. Ni wewe unaweza kuyapa thamani na ni wewe unaweza kuyafanya yasiwe kitu. Anza kila kitu kwa ajili ya kuleta furaha katika maisha yako.

Hakuna raha ya kuishi kama huna amani. Sasa ni kwanini fulani akuondolee raha ya maisha ikiwa mapenzi ni kwa ajili ya kufurahia maisha? Kubali kuumia kwa muda fulani ili utengeneze furaha na amani ya muda mrefu katika maisha yako. Kuanza upya si ujinga, ila ni kuamua kubadili upepo wa maisha yako.

ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -