Saturday, January 16, 2021

ARISTICA CIOABA: ATAIOKOA AU KUIPOTEZA ZAIDI AZAM FC

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

WINFRIDA MTOI NA ABDUL KHALID (TSJ)

WIKI iliyopita klabu ya Azam FC ilimtangaza kocha mpya Aristica Cioaba, atakayekinoa kikosi hicho kwa miezi sita akichukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Mhispania, Zeben Hernandez.

Kocha huyo raia wa Romania, kabla ya kutua Azam alikuwa anakinoa kikosi cha Aduana Stars nchini Ghana aliyoiacha ikiwa imemaliza kwenye nafasi ya pili katika ligi ya nchini humo.

Licha ya kutokuwa maarufu sana lakini wasifu wa kocha huyo unaonyesha kuwa amepita katika klabu mbalimbali akiwa kama kocha mwenye taaluma kubwa ya soka, akiwa anamiliki leseni B ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Soka barani Ulaya, (UEFA).

Hivyo kama ulijua kocha huyu ni wa kuchezea, umeumia kwa sababu wasifu wake unaonyesha timu zote alizopitia aliziacha zikiwa katika nafasi nzuri.

Cioaba alipata leseni A mwaka 2005 baada ya mafanikio ya kupata ile ya B mwaka 2004 kutoka Shirikisho la Soka la nchini Romania.

Unajua kazi ya ukocha alianzia wapi?

Kazi yake ya ukocha alianzia nchini Morocco katika klabu ya Raja Casablanca, ambapo alifanya kazi kama msaidizi wa kocha Alexandru Moldovan msimu wa mwaka 2005 hadi 2006.

Katika mwaka wake mmoja aliokaa katika klabu hiyo kama kocha msaidizi, aliweza kuisaidia timu yake hiyo kuchukua kombe la ligi msimu wa 2005-2006 na kuweza kufika katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2005.

Mwaka 2006 alihamia nchini Misri katika klabu ya Al-Masry inayoshiriki ligi kuu nchini humo, ambapo pia alifanya kazi akiwa kama kocha msaidizi, chini ya kocha huyo huyo aliyeanza naye Moldovan.

Hata hivyo, mwaka 2007, Cioaba alirejea nchini kwao Romania ambapo aliteuliwa kuwa kocha mkuu katika klabu ya FC Bals iliyokuwa ikishiriki Ligi Daraja la Tatu na kudumu nayo hadi mwaka 2009 kabla ya kuhamia nchini Kuwait.

Bado kocha wake Moldovan aliendelea kumhitaji katika kazi zake, kwani alipokuwa Kuwait walikutana tena katika klabu ya Al-Tadamun iliyokuwa ikishiriki ligi kuu nchini humo.

Kocha huyu inaelekea hapendi kukaa sehemu muda mrefu, kwani Ligi ya Kuwait ilipomalizika alihamia katika nchi ya Jordan iliyopo Magharibi mwa Bara la Asia mwaka  2010 na kujiunga na klabu ya Shabab Al-Ordon  inayoshiriki Ligi Kuu ys Jordan kama kocha mkuu.

Katika kipindi kifupi alichoitumikia klabu hiyo, alifanikiwa kuifikisha katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA nchini humo mwaka 2011-2012, ambapo walitolewa kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya timu ya Al-Faisaly SC.

Mwaka 2011, alitoka Bara la Asia na kujerea tena Afrika, moja kwa moja akitua nchini Ghana na kujiunga na timu ya Aduana Stars akichukua nafasi ya Herbert Addo aliyoisaidia kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika CAF licha ya kutolewa mapema.

Kama kawaida yake, mwaka mmoja ulipoisha alihamia Oman na kuwa kocha mkuu wa timu ya Saham SC na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2011/2012.

Timu hiyo ilifanikiwa kupanda katika ligi kuu ya nchini Oman msimu wa 2012-2013 na kushika nafasi ya pili katika Kombe la Shirikisho nchini humo.

Akiwa Oman, ziliibuka taarifa kuwa kocha huyo anatarajia kurudi Ghana kuifundisha timu ya Medeama kwa mkataba wa miaka miwili na nusu, lakini dili hilo lilishindikana na kubakia nchini humo ambapo alijiunga na klabu ya Al-Oruba.

Hata hivyo, hakudumu sana na alirejea klabu yake ya Saham, Juni 2015 na kusaini mkataba wa mwaka mmoja ikiwa inashiriki ligi kuu. Katika timu hiyo wanamkumbuka kwa kuifunga Bidia SC mabao 9-0 timu inayoshiriki Ligi Daraja la Pili na kufanikiwa kutinga katika hatua ya robo fainali ya Kombe la Sultani Qaboos katika msimu wa 2015-2016.

Lakini Januari, 2016, uongozi wa klabu ya Saham waliamua kumwachia Mromania huyo baada ya mkataba wake kufikia tamati, ambapo alirudi katika klabu ya Aduana Stars kama kocha wa muda kabla ya kupewa mikoba ya moja kwa moja.

Amekuja akiikuta Azam ambayo ilivurugwa na mfumo wa Wahispania, lakini katika siku za karibuni ameishuhudia ikiwa timu bora chini ya Idd Nasooro Cheche, ambaye ameiwezesha kutwaa Kombe la Mapinduzi.

Azam kwa sasa inaonekana ni timu inayocheza kwa mipango na uelewano mkubwa chini ya falsafa ya Cheche, ubora wake ambao bila shaka utaanza kuonekana kwenye ligi kuu huenda ukalazimika kufumua mfumo uliopo sasa na kuingia mfumo mpya ambao kocha anauamini.

Je, nini kitatokea chini ya Mromania huyu? Kuiona Azam ikipaa zaidi ya hapa alipoiweka Cheche au tushuhudie Azam mpya ambayo itaanza tena kujifunza mifumo na falsafa mpya za Kiromania ambazo zitagharimu miezi kadhaa?

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -