Wednesday, October 28, 2020

Arsenal ina kazi mbili; kufuta historia kwa Chelsea, mwamuzi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

LEO mbio za kufukuzia taji la Ligi Kuu England zitapambwa na mtanange mkali kati ya Chelsea na Arsenal.

Mwamuzi Michael Oliver, ndiye atakayesimama katikati ya uwanja katika mchezo huo wa ‘London Derby’.

Wakiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Emirates, Arsenal watawakaribisha wababe hao wa Magharibi mwa London.

Gunners hawajatamba mbele ya Chelsea katika michezo ya ligi tangu walipoibuka na ushindi wa mabao 5-3 mwaka 2011.

Lakini huenda rekodi hiyo ikaendelea kutokana na historia mbaya ya Arsenal wanapokutana na mwamuzi Oliver.

Katika michezo nane iliyopita ya ligi iliyochezeshwa na Oliver, Arsenal hawajashinda hata mmoja.

Mbele ya mwamuzi huyo, wakali hao wa Kaskazini mwa London, wameambulia sare tano na vichapo vitatu.

Oliver ndiye aliyechezesha mchezo wa ufunguzi wa ligi msimu huu ambapo Arsenal walichapwa mabao 4-3 dhidi ya Liverpool.

Arsenal wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kujikusanyia pointi 10.

Wapinzani wao Blues wanakamata nafasi ya tatu wakiwa na idadi hiyo ya pointi, wakizidiwa kwa tofauti ya mabao.

Kwa upande wa Cheslea, hawajapoteza mchezo katika mechi 13 zilizopita.

Katika mtanange wa leo, Cesc Fabregas ambaye aliwahi kuwa nahodha wa Gunners anatarajiwa kuingia katika kikosi cha kwanza hasa baada ya kupasia nyavu mara mbili katika mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Leicester City.

Kocha Arsene Wenger ataingia kwenye mchezo huo bila huduma ya kiungo wake, Aaron Ramsey, ambaye ni majeruhi.

Huenda safu ya kiungo ya Mfaransa huyo ikamtegemea zaidi Granit Xhaka ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri katika siku za hivi karibuni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -