Monday, January 18, 2021

Arsenal, mmeshampata mrithi wa Wenger?

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

LICHA ya Arsene Wenger kutumia muda wa miaka 20 akiwa kama kocha wa Arsenal, amekuwa na kipindi kigumu katika miaka ya hivi karibuni, hasa kwenye suala la mkataba wake na wababe hao wa London Kaskazini.

Kwa yote aliyoyafanya kwa ajili ya kuiweka timu hiyo sawa katika maeneo mbalimbali, kuna kipindi ambacho suala la kuongeza muda ndani ya mkataba wake limekuwa likipata mitikisiko ya hapa na pale.

Katika miaka 10 ya mwanzo akiwa kama Kocha wa Arsenal, Wenger aliwahi kutakiwa na timu mbalimbali kubwa za Ulaya, lakini Mfaransa huyo aliamua kusaini mkataba mpya kuanzia 2007 hadi 2011, huku mpango wa uwanja mpya wa Emirates ukiwa ndio chachu ya yeye kufanya hivyo.

Mwaka 2010 aliongeza mkataba hadi 2014 na ndani ya miaka hiyo minne ndipo manung’uniko juu ya Wenger yalipoanza, kwani timu ilianza kuhaha kiuchumi, hali iliyowapelekea kushindwa kuwania mataji ipasavyo na kuendana na ile historia yao ya kutesa miaka ya nyuma.

Mashabiki wengi wakataka kumwona kocha mpya kwenye benchi la ufundi kwa wakati huo.

Hata hivyo, mwaka 2014 mwelekeo wa upepo ulianza kubadilika ndani ya timu hiyo. Uchumi ukaanza kuridhisha, mikataba mipya ya udhamini na jezi ikaiongezea Arsenal nguvu ya kutumia fedha za kutengeneza timu imara, lakini bado suala la kutochukua mataji kwa miaka yote hiyo likaamsha tena manung’uniko.

Fununu za kukamilika kwa makubaliano kati ya Arsenal na kocha mwingine nazo ziliibuka, lakini kwa sababu tu ya klabu kuwa kwenye hatua za lala salama kuelekea kunyakua taji la FA, dili hilo likapotea kabisa.

Nusu fainali ya michuano hiyo wakakutana na Wigan kwenye dimba la Wembley, mchezo ulikuwa mgumu mno, huku Arsenal ikibakiwa na dakika nane tu za kujiokoa na kichapo kabla ya beki Per Mertesacker kufunga bao la kusawazisha dakika za mwisho na mchezo kwenda kwenye dakika za nyongeza na Arsenal ikashinda kwa penalti kabla ya kuifunga Hull City mabao 3-2 kwenye fainali.

Zile kelele za mashabiki ambazo zilikuwa na nguvu kubwa ya kuzuia mkataba wowote mpya usisainiwe, zilizimika ghafla baada ya Wenger kuiongoza timu kushinda taji la FA na akasaini mkataba mpya.

Arsenal ikafululiza tena kutwaa taji hilo mwaka 2015, na ilikuwa wazi kwamba mfululizo huo ungekuwa chachu kubwa kwao kunyakua na lile la Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini kwa mara nyingine tena timu hiyo ikateleza na kuliachia taji kwa Leicester City.

Baadhi ya mashabiki wa Arsenal wanadhani muda umefika wa kubadilisha kocha atakayeipeleka timu kwenye mwelekeo mpya.

Manung’uniko yote hayo yakapungua na wakabaki mashabiki wachache waliotaka kocha mpya baada ya mkataba wa Wenger kumalizika.

Na bado kutakuwa na mashaka kidogo juu ya Wenger kutaka kubakia kikosini.

Stori ziliibuka kwamba huenda akapewa kibarua cha kuinoa England, lakini ukweli ni kwamba kwa mtu mwenye mapenzi makubwa na soka kama Wenger hatakuwa na maisha marefu kwenye soka la kimataifa.

Hata bodi ya Arsenal imekuwa ikimkubali Mfaransa huyo, akiwemo mmiliki Stan Kroenke na mwanahisa Alisher Usmanov.

Na kama hiyo haitoshi, ndani ya bodi ya Arsenal kuna udhaifu kidogo katika ujuzi wa masuala ya soka (kutojua nini kinachohitajika zaidi) na kinachojulikana humo ni kuongeza tu mkataba wa Wenger.

Hata hivyo, klabu pamoja na kocha mwenyewe wanajua kabisa kwamba mkataba mpya unatakiwa uwe na kipengele kinachogusia mipango ya kweli ya kusaka mafanikio, hata kama timu inacheza Ligi ya Mabingwa Ulaya kila msimu.

Kumaliza nafasi ya pili msimu uliopita inaweza kuwa sababu nyingine ya kujifurahisha, lakini walikuwa na sababu ya kuwa mabingwa pia.

Yote hayo yanajulikana ndani ya Arsenal, ndiyo maana klabu pamoja na Wenger wanajua kuna muda sahihi na usio sahihi wa kutangaza mkataba mpya na si muda huu hata kama timu ipo kwenye mwelekeo mzuri.

Kama mambo yakienda kombo tena, Wenger anaweza kujikuta akipata shida tena kama yale yaliyomtokea mwaka 2014.

Atatimiza umri wa miaka 67 ifikapo Oktoba 22, mwaka huu, ana muda mfupi sana uliobaki kwenye maisha ya soka, lakini hata mapenzi yake na Arsenal yana muda mfupi pia. Hakuna namna, mrithi wake inabidi atafutwe mapema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -