Tuesday, October 27, 2020

Arsenal wana dalili zote za kubeba taji England

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

LONDON, England

USHINDI wa mabao 4-1 walioupata Arsenal mwishoni mwa wiki iliyopita haukuwa pekee mwiba kwa kocha David Moyes, ambaye amekuwa na mwanzo mbaya na kikosi hicho cha Sunderland msimu huu katika historia ya Ligi Kuu England, lakini umeonyesha kwamba Gunners wanataka taji la ligi hiyo ambalo hawajaligusa tangu mwaka 2004.

Mabao matatu waliyofunga ndani ya dakika saba katika kipindi cha pili yaliimaliza Sunderland wakionekana kutumia uwezo wao wakati unaohitajika.

Mshambuliaji Olivier Giroud, aliingia kucheza dakika 21 za mwisho na kukiweka kikosi hicho cha Moyes kwenye hatari ya kushuka daraja na kuna sababu saba kwanini unaweza ukawa mwaka wa Arsenal.

 

  1. wameanza vizuri

Sasa hivi Gunners wana pointi 23 walizokusanya katika mechi zao 10 za mwanzo wa Ligi Kuu England na ni mara nne pekee wamefanikiwa kufanya hivyo.

Wakati walipoibuka kuwa mabingwa wa mwaka 1998, walikusanya jumla ya pointi 22 baada ya mechi 10 na mwaka 2004, ambapo walimaliza msimu bila ya kufungwa walikusanya pointi 24 kwa mechi 10 pia.

Pamoja na kupoteza mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na kuruhusu mabao kwenye mechi kama dhidi ya Watford, Southampton, Swansea  na Sunderland lakini kihesabu wako vizuri na sasa wako kileleni nyuma ya Manchester City wakiwa sawa kwa pointi wakizidiwa mabao mawili na vinara hao.

 

2.KIKOSI KIPANA

Giroud ametokea benchi na kupachika mabao mawili ndani ya dakika tano, lazima hilo litawatisha wapinzani wa Arsene Wenger.

Kama amepumzishwa chipukizi Alex Iwobi, kisha kuingizwa mkali wa mabao wa Gunners, Giroud kuingia na kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho. Aaron Ramsey, akiwa amerejea kikosini, huku Alex Oxlade-Chamberlain akionyesha kiwango.

Pamoja na wachezaji hao huku Wenger akiwa na nyota wengine waliokuwa majeruhi kama Theo Walcott, Lucas Perez, kiungo Santi Cazorla na beki Nacho Monreal, lakini bado walionekana kuwa vizuri.

Huku wakiwa na chipukizi wao wanaofanya vizuri kwenye Kombe la Ligi, hiyo inaonyesha jinsi kikosi hicho kilivyo na wachezaji wa kutosha.

 

  1. SAFU YA ULINZI

Mkongwe wa klabu hiyo, Thierry Henry, anajua jinsi ambavyo alikuwa akiwasumbua mabeki wa Arsenal kwenye uwanja wa mazoezi alipokuwa bado kwenye kikosi hicho akijifunza ukocha.

Lakini kabla ya mechi hiyo dhidi ya kikosi cha Moyes mjini Wearside, mchambuzi huyo wa Ufaransa alizungumzia ukuta wa timu yake hiyo ya zamani inayojengwa na mabeki wa kati mahiri, Shkrodan Mustafi na Laurent Koscielny. Calum Chambers, ametolewa kwa mkopo akapate uzoefu, chipikizi Rob Holding, amekuwa akipangwa pamoja na Paulista kupata uzoefu.

Kuumia kwa goti kwa nahodha Per Mertsacker, kumemfanya beki mpya aliyesajiliwa majira ya kiangazi, Mustafi na beki wa Ufaransa, Koscienly kucheza pamoja na kutengeneza kombinesheni ambayo ngumu kuipenya.

 

  1. WANAJIFUNGA WENYEWE

Bao kama la Sunderland lingeweza kuzuilika na hicho ndicho kinachowafanya kushindwa kukaa juu ya msimamo wa Ligi Kuu England, kutokana na kuruhusu mabao pale wanaposhindwa kuwa makini.

Udhaifu wao wa kucheza mipira ya adhabu unapaswa kufanyiwa kazi na kudhibiti kuruhusu kufungwa mabao mepesi kama bao la penalti walilofungwa na Jermain Defoe, baada ya makosa yao wenyewe.

Wamekuwa wakicheza kwa uhuru wanavyotaka wao, lakini mara kadhaa wamekuwa wakipata matatizo kwa makosa yao.

Labda wanajisahau kwa jinsi wanavyotawala mchezo na kuwafanya wapoteze umakini, lakini vyovyote itakavyokuwa wanapaswa kuwa makini na kutoruhusu mabao na kushinda mabao mengi kadiri wanavyoweza.

 

  1. UBORA WA MASTAA

Mesut Ozil na Sanchez wanafanya mambo makubwa. Mwanzoni nyota huyo wa Chile alikumbwa na majeruhi na kiungo wa Ujerumani, Ozil kushindwa kutakata kwenye mechi kubwa, lakini kwa sasa wanaonekana kuwa ni kati ya wachezaji bora wa Ligi Kuu England.

Wakati Sanchez anapokuwa fiti kikweli kweli hawezi kukabika, akichanganya na uwezo wake na bidii amekuwa akiwasumbua sana mabeki.

Ozil anafanya mambo makubwa anapokuwa na viungo kama Mohamed Elneny, Francis Coquelin na Oxlade-Chamberlain wakimzunguka, hatakiwi kufanya kazi kubwa sana.

Wachezaji hao wawili wanaweza kupata namba kwenye kikosi chochote cha Ligi Kuu England kutokana na kiwango chao na ni wachezaji wachache walio kwenye ubora wao kwa wakati huu. Liverpool na Tottenham wanafanya vizuri kwa sababu ya makocha wao ambao wanaendelea na njia walizotumia kununua vikosi vyao vizuri.

Pamoja na Man City kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya West Brom, lakini bado wako kwenye kipindi kigumu, huku Manchester United na Chelsea wakionekana kuwa kwenye kipindi cha mpito. Lakini kwa sasa wachezaji hao wawili wa Arsenal wako vizuri na lazima wapinzani wao watakuwa wanaingia presha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -