Friday, December 4, 2020

ARSENAL WANA GUNDU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

*Kukutana kati ya Bayern, Leverkusen, Madrid, Dortmund, Juventus au Sevilla

LONDON, England

Arsenal wamefanikiwa kumaliza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wakiwa kileleni mwa Kundi A, baada ya kuichapa Basel mabao 4-1 juzi Jumanne.

Ingawa wamefanikiwa kumaliza nafasi hiyo ya juu ili kukwepa vigogo wengine Ulaya, lakini ni kama wamekuwa na gundu kwa kuwa vigogo hao wengi wamemaliza nafasi ya pili na kuna uwezekano wa kukutana nao kama miaka mingine.

Kuanzia mwaka 2011 hadi msimu uliopita, Arsenal wamekuwa wakishika nafasi ya pili, inayosababisha na kukutana Barcelona na Bayern Munich, ambazo zote amekumbana nao mara mbili mbili katika kipindi chote hicho.

Msimu huu baada ya kumaliza nafasi ya kwanza, wanatarajiwa kukutana na kati ya Bayern Munich na Bayer Leverkusen au Real Madrid na Borussia Dortmund, asipoanguka mikononi mwa timu hizo anaweza akakumbana Juventus au Sevilla.

Jambo la kujiuliza ni kwamba wataweza kuvuka hatua hiyo ya mtoano na kuingia robo fainali Ulaya, kulingana na timu ambazo anaweza kukutana nazo hatua ya mtoano.

Ambapo jambo la kutia shaka zaidi kwa Arsenal ni kiwango chao wanapokumbana na klabu kubwa baada ya kutoka sare mbili na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, huku wakifungwa na Liverpool wakitoka sare na Tottenham na Manchester United Ligi Kuu England.

Hivyo kuifunga Basel na Ludogorets mara mbili kila moja halikuwa jambo kubwa kwao kwa kuwa timu ndogo kama hizo zimekuwa hazina madhara kwa Arsenal tofauti na timu kubwa na hilo ndilo linaloonyesha kwamba nafasi yao ya kusonga mbele kuwa ni finyu kwenye michuano hiyo.

Kwa upande wa Ligi Kuu England, Gunners wamemudu kwenda sambamba na Chelsea na Liverpool. Huku mwezi wao wa kihistoria na mgumu kwao Novemba umepita tofauti na miaka yote wakiendelea kuwa kwenye nafasi nzuri. Ambapo katika mwezi huo Novemba kikosi hicho cha Arsene Wenger kimefungwa mechi moja ya Kombe la Ligi (EFL Cup), lakini wametoka sare mechi tatu.

Lakini kikosi hicho cha Wenger kinaweza kuvuka hata ikikutana na Real Madrid, baada ya kuwahi kuifunga klabu hiyo ya Hispania kwenye hatua ya mtoano mwaka 2006. Kama Arsenal wanataka kuvuka hatua hiyo ya 16 bora na kufika hadi fainali itategemea na jinsi watakavyocheza mechi zao wanazokutana na timu kubwa.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa UIaya juzi Jumanne, mshambuliaji wa Arsenal, Lucas Perez alitakata na kupiga ‘hat-trick’.

‘Hat-trick’ hiyo ya Perez na bao moja la Alex Iwobi lilisaidia Arsenal kupata ushindi huo wa mabao 4-1 dhidi ya Basel, huku Ludogorets wakiibana Paris Saint-Germain na kutoka sare ya mabao 2-2 mjini Paris nchini Ufaransa na kuifanya klabu hiyo ya London kumaliza wakiwa vinara wa kundi hilo kwa mara ya pili ndani ya miaka mitano. Pamoja na ushindi huo pia walifanikiwa kumaliza hatua hiyo ya makundi bila ya kufungwa kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2005-06, ambapo walifanikiwa kutinga fainaila.

Mchanganyiko wa kikosi kilichopangwa na Wenger katika mechi hiyo, safu ya ulinzi ikiongozwa na Laurent Koscinly akishirikiana na Rob Holding, huku Gabriel Paulista akicheza upande wa kulia na Kieran Gibbs kushoto, ilionekana kuwa makini pamoja na kuwapumzisha akina Shkodran Mustafi, Nacho Monreal na Hector Bellerin akiwa majeruhi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -