Thursday, October 22, 2020

Arsenal yaitaka Chile imrejeshe Sanchez

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

LONDON, England

ARSENAL wanataka Alexis Sanchez arejee London baada ya mshambuliaji huyo kupata majeraha juzi Jumanne.

Sanchez alipata majeraha ya kigimbi wakati akiwa mazoezini na timu yake ya Taifa ya Chile na atakosa mechi ya leo kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 dhidi ya Colombia.

Chile wanataka kumbakiza mshambuliaji huyo wakiwa na matumaini kwamba ataweza kucheza mechi yao ijayo dhidi ya Uruguay wiki ijayo.

Majeraha hayo ya Sanchez yamefanyiwa vipimo na timu ya madaktari wa timu hiyo ya taifa ya Chile, lakini Gunners wanataka kumchunguza mchezaji huyo wenyewe.

Lakini Chile walidai kwamba majeraha ya mchezaji huyo si ya kutisha sana, lakini Arsenal hawataki Sanchez acheze dhidi ya Uruguay, Jumanne ya wiki ijayo na kurejea London kwa ajili ya matibabu.

Ikiwa itawezekana, kocha wa Gunners, Arsene Wenger, anataka Sanchez kuwamo kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United, Jumamosi ya wiki ijayo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -