Thursday, October 22, 2020

Asya Idarous alivyofunika Shikamoo Swahili Fest Marekani

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

NA MWANDISHI WETU,

Mkongwe wa mitindo ya mavazi nchini Tanzania, Asya Idarous ‘Mama wa Mitindo’, mwishoni mwa wiki iliyopita alitia fora kwenye onyesho kubwa la mavazi nchini Marekani.

Onyesho hilo, lililopewa jina la Shikamoo Swahili Festival, lilifanyika mjini Atlanta, Georgia na mbunifu huyo mkongwe kupata fursa ya kuonyesha mavazi yake ya kitamaduni za Kiswahili.

Lengo la onyesho hilo la mavazi ambalo liliambatana na shughuli mbalimbali za kitamaduni, lilikuwa ni kuenzi Kiswahili kama Afrika Mashariki pamoja na tamaduni zake.

Pamoja na maonyesho hayo ya mavazi kwa wakubwa, pia kulikuwa maonyesho ya mavazi ya watoto na majadiliano kwa lugha ya Kiswahili, ambapo watu mbalimbali walijifunza maneno mbalimbali ya Kiswahili, wakiulizana maswali na kuwekana sawa juu ya matumizi mbalimbali ya lugha hiyo.

Mashabiki mbalimbali wa mavazi waliohudhuria walipata fursa ya kula vyakula mbalimbali vya kiswahili, pamoja na kushiriki michezo mbalimbali ya kitamaduni kama kucheza ngoma za asili.

Vikundi mbalimbali vya ngoma za kitamaduni zinazotumia lugha ya Kiswahili kutoka Tanzania na Burundi vilitoa burudani kwenye onyesho hilo la Shikamoo Swahili Festival.

Mavazi mbalimbali kama kanga na vitenge yalionyeshwa katika tamasha hilo, ambapo wanamitindo mbalimbali walipanda jukwaani na kupita mbele ya mashabiki wa mavazi.

Nguo mbalimbali zilizobuniwa na mama huyo wa mitindo nchini zilionekana kuwavuta mashabiki hao, waliokuwa wakipiga makofi na wakishangilia muda wote.

Pia mashabiki hao walitumia fursa hiyo kununua mavazi hayo ya kitamaduni kwa ajili ya matumizi yao binafsi, ambapo baadhi ya mavazi yaliyonunuliwa kwa wingi yalikuwa ni mabaibui ya zamani.

Zawadi mbalimbali zilitolewa baada ya onyesho hilo, kama sehemu ya kunogesha Shikamoo Swahili Festival, ambapo mashabiki waliohudhuria wameomba lifanyike kila mwaka, ili kudumisha na kuendeleza lugha hiyo ya Kiswahili, ambayo iliwafanya kukutana pamoja nchini Marekani.

Akizungumzia onyesho hilo, Asya alisema amefurahishwa na mapokezi aliyopata kutoka kwa mashabiki pamoja na maandalizi mazuri yaliyofanywa na wenyeji wake, Rahima Shaaban na Maryam Haiti.

“Tamasha lilikuwa zuri na nimefurahishwa na mapokezi kutoka kwa mashabiki na wenyeji wangu wameandaa vizuri onyesho hilo. Pia nitoe pongezi kwa wanamitindo walioshiriki, wamefanya kazi nzuri kuwavutia mashabiki,” alisema Asya.

“Huu ni mwanzo mzuri kwa onyesho hili, watu wamevutiwa na ubunifu wa nguo zangu na kuzinunua, hasa mabaibui yale ya kizamani.

“Ilikuwa fursa nzuri kwa watu wa Afrika Mashariki kudumisha lugha ya Kiswahili, lakini wapo watu wengine nje ya Afrika walipata fursa na wao kujifunza lugha yetu, lilikuwa jambo zuri kwa kweli,” aliongeza mbunifu huyo, ambaye amekuwa akifanya maonyesho mbalimbali nchini Marekani na kwa hapa nchini amekuwa akiandaa maonyesho kama Lady in Red, Kanga Party na mengineyo mengi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -