Tuesday, October 27, 2020

Atletico ililamba dume kwa mastraika hawa

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

MADRID, Hispania

KWA miaka kadhaa sasa, Atletico Madrid imekuwa mshindi barani Ulaya kwa kuibuka na mastraika wakali.

Huku klabu nyingine zikihaha katika safu ya ushambuliaji, kwa Atletico umekuwa ni mchezo mdogo tu.

Hivi sasa wana Mfaransa, Antonio Griezmann, ambaye amekuwa kwenye ubora wa juu katika siku za hivi karibuni.

Mbali na Geriezmann, wafuatao ni baadhi ya wapachikaji mabao hatari ambao waliwahi kutokea.

  1. Christian Vieri

Kutokana na umahiri wake wa kupasia nyavu, Muitalia Vieri alijijengea heshima kubwa alipokuwa Atletico.

Alitua Atletico akitokea Juventus na uhamisho wake uligharimu euro milioni 10 pekee.

Ingawa aliichezea Atletico msimu mmoja pekee, nyota huyo alifunga jumla ya mabao 24 katika mechi 24 za La Liga.

Katika mechi za mashindano yote, alipasia nyavu mara 29 katika michezo yake 32.

Kutokana na uwezo wake huo, alichukuliwa na Lazio kwa ada ya euro milioni 25.

  1. Jimmy Floyd Hasselbaink

Hasselbaink naye ni miongoni mwa mafowadi waliojenga jina wakiwa na Atletico.

Alihamia Hispania akitokea England alikokuwa akikipiga katika klabu ya Leeds kwa pauni milioni 10.

Mholanzi huyo aliichezea Atletico michezo 34 na kupachika mabao 24.

Katika msimu wake wa kwanza, staa huyo alishika nafasi ya pili kwenye orodha ya wapachikaji mabao, lakini Atletico ilishuka daraja.

Alifunga mara mbili katika mchezo wa ‘Madrid derby’ dhidi ya Real Madrid na kwa mara ya kwanza Atletico waliibuka na ushindi kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu kwa kipindi cha miaka tisa.

Alipoondoka La Liga, Hasselbaink alirejea England ambako alijiunga na Chelsea.

  1. Fernando Torres

Mpaka leo Torres ni kipenzi cha mashabiki wa Atletico.

Alikulia pale na kupata umaarufu akiwa na klabu hiyo.

Alitumia misimu saba akiwa na Atletico.

Katika msimu wake wa kwanza akiwa kikosi cha kwanza akitokea kwenye ‘academy’ ya klabu hiyo, alifunga mabao 13 katika mechi 29. Kipindi hicho alikuwa kinda wa umri wa miaka 18.

Msimu wake wa pili ulishuhudia akipasia nyavu mara 19 katika mechi 35 na ndipo aliposhika nafasi ya tatu kwenye orodha ya wapachikaji mabao.

Akiwa na umri wa miaka 19, tayari Torres alishakabidhiwa kitambaa cha unahodha.

Mwaka 2007, alisajiliwa na Liverpool ambako alithibitisha makali yake kabla ya kuhamia Chelsea ambako alishindwa kutamba.

Kwa sasa Torres amerejea katika klabu yake hiyo ya zamani, Atletico.

  1. Sergio Aguero

Muargentina huyo alitua Atletico akitokea Independiente.

Ada yake ya uhamisho ya euro milioni 23 ilivunja rekodi ya usajili pale Atletico.

Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu kabla ya mabosi wa Atletico kukiri kuwa hawakukosea kumchukua fowadi huyo.

Kwa kipindi chote alichokaa klabuni hapo, Aguero alipachika jumla ya mabao 74 katika michezo 175 aliyoshuka dimbani.

Kwa msaada wake wa kuwatungua walinda mlango, katika msimu wa 2009-2010, Aguero aliiongoza Atletico kushinda taji la Ligi ya Europa na kufika fainali ya Copa Del Rey.

Msimu uliofuata, alicheka na nyavu mara 20 na hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kufikisha idadi hiyo katika maisha yake ya soka.

Mfanikio hayo yaliwavutia Manchester City, ambao walitoa euro milioni 45 kumng’oa Atletico.

  1. Diego Forlan

Forlan alikuwa moto wa kuotea mbali mbele ya makipa wa timu pinzani.

Katika msimu wake wa kwanza, raia huyo wa Uruguay alipasia nyavu mara 23.

Alifunga mabao 32 katika mechi 33 katika msimu wake wa pili.

Alipotimka Atletico mwaka 2011, Forlan alitua Italia na kujiunga na Inter.

  1. Radamel Falcao

Akiwa Atletico, Falcao alikuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa timu pinzani.

Aliposajiliwa na Atletico kwa ada ya euro milioni 40, straika huyo raia wa Colombia alikuwa ndiye mchezaji ghali kuliko wote pale Atletico.

Kwa kiasi kikubwa, aliwasahaulisha mashabiki wa Atletico kuondoka kwa Forlan na Aguero.

Falcao aliwashangaza mashabiki wa Atletico kutokana na umahiri wake wa kupasia nyavu ambapo alifunga mabao 52 katika michezo 68.

Akatupia ‘hat trick’ katika mchezo wa UEFA Super Cup dhidi ya Chelsea.

Akaiwezesha Atletico kushinda taji la Copa Del Rey.

Baadaye, Falcao alihamia Monaco, huku ada ya uhamisho wake ikitajwa kuwa ni euro milioni 60.

  1. Diego Costa

Kama ilivyokuwa kwa wenzake, Costa naye aliingia kwenye historia ya Atletico kutokana na umahiri wake wa kucheka na nyavu.

Akiwa kwenye ubora wake, aliiwezesha Atletico kunyakua taji la La Liga pamoja na kuifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kiwango alichokionesha katika mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Chelsea, kiliwafanya wababe hao wa Magharibi mwa London kumsajili.

Akiwa na ‘uzi’ wa Atletico, mkali huyo alipachika jumla ya mabao 43 katika michezo 94 aliyocheza.

Alipofunga jumla ya mabao nane kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, aliifikia rekodi iliyowekwa na Vava mwaka 1959 ambaye pia aliwahi kutesa na Atletico.

  1. David Villa

Akishirikiana na Costa, Villa alifanya kazi kubwa pale Atletico, hasa katika msimu wa 2013-14.

Ndiye mfungaji wa muda wote wa timu ya Taifa ya Hispania.

Alitoka Barcelona na kujiunga na Atletico katika msimu wa 2013-14.

Atletico walitumia kiasi cha euro milioni 5 pekee kumsajili Villa.

Mabao yake 13 katika mechi 36 yaliiwezesha Atletico kushinda taji la La Liga mbele ya Madrid na Barca.

  1. Mario Mandzukic

Alikuwa nyota wa mchezo wakati Atletico walipoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Madrid.

Alisajiliwa na Atletico mwaka 2014 kuchukua nafasi ya Costa.
Mpaka anatimka Atletico, Mandzukic alikuwa na jumla ya mabao 20 katika mechi 43.

Alicheza kwa msimu mmoja kabla ya kununuliwa na Juventus kwa euro milioni 19.

  1. Antoine Griezmann

Ndiye kila kitu kwenye safu ya ushambuliaji ya Atletico kwa sasa.

Kabla ya kuwa mshambuliaji wa kati, Mfaransa huyo alikuwa akicheza kama winga.

Mpaka sasa, ameshapachika zaidi ya mabao 30 katika takribani michezo 50 aliyoichezea Atletico.

Atletico walitoa pauni milioni 24 pekee kumsajili staa huyo wa zamani wa Real Sociedad, lakini sasa wanaweza kuingiza mara nne ya kiasi hicho kama wataamua kumpiga bei.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -