Monday, August 10, 2020

ATUPELE GREEN AZIITA KLABU MEZANI

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MAREGES NYAMAKA

SIKU chache baada ya kutupiwa virago aliyekuwa mshambuliaji wa Singida United, Atupele Green, ameziita klabu zinazohitaji huduma yake mezani na kufanya mazungumzo.

Jumatatu klabu ya Singida ilitangaza kuachana na wachezaji wake watatu, akiwamo mshambuliaji huyo waliyemsajili Mei mwaka huu akitokea JKT Ruvu iliyoshuka daraja, yakiwa ni matakwa ya kocha Hans Van der Pluijm.

Atupele hadi anatupiwa virago alikuwa hajafanikiwa kuifungia timu yake hiyo bao, katika mabao matano yaliyofungwa na timu ndani ya michezo 11 ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na BINGWA, Atupele alisema mchezaji kuachwa katika timu ni kitu cha kawaida, anachokifanya ni kuzikaribisha klabu nyingine kufanya naye mazungumzo kwani bado ana uwezo wa kupambana uwanjani kutimiza jukumu lake hilo la kufunga.

“Sichagui timu ya kuchezea kikubwa ni makubaliano katika mkataba wa pande zote mbili, klabu ambayo iko tayari tuonane, mpira ndio kazi yangu yaliyopita yamepita tugange yajayo,” alisema.

Nyota huyo aliyewahi kuichezea Ndanda ya mkoani Mtwara, miongoni mwa mafanikio aliyoyapata katika soka ni kutwaa kiatu cha dhahabu baada ya kuibuka mfungaji bora wa Kombe la Azam Sports Federation msimu wa 2015/16.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -