Saturday, November 28, 2020

AWUDU ZAKARI; Straika Mghana anayenukia Stand

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MARTIN MAZUGWA

KADIRI siku zinavyozidi kwenda ndivyo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  Bara inavyozidi kuimarika kutokana na kuvutia wachezaji wengi wa kimataifa ambao wamekuwa wakimiminika nchini kujaribu kusaka klabu za kuchezea.

Ili kupambana na wimbi la wachezaji wa kimataifa ambao wamekuwa wakimiminika nchini kila kukicha, Shirikisho la soka Tanzania (TFF) limeamua kubana idadi ya wachezaji wa kigeni katika klabu za VPL ambapo kila klabu ina ruhusa ya kusajili wachezaji saba tu wa kigeni.

Lakini pamoja na TFF kuweka kiwango maalumu cha idadi ya wachezaji wa kigeni kusajiliwa VPL, bado mastaa kutoka kila kona ya Afrika wanamiminika nchini kujaribu bahati yao.

Mmoja kati ya wachezaji ambao wako nchini kwa sasa kusaka timu ya kuchezea kwenye mzunguko wa pili wa VPL, ni Awudu Zakari straika wa kimataifa wa Ghana ambaye aliwahi kuitoa udenda Yanga.

Staa huyo ambaye yuko nchini kwa ajili ya kujaribu bahati yake kwenye klabu ya Stand United, hivi karibuni alipiga stori na BINGWA na kuweka wazi mambo mengi kuhusu maisha yake binafsi na soka kwa ujumla.

Mahojiano hayo na Zakari aliyewahi kukipiga katika klabu ya Nogoom el Mostakbal inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri akicheza sambamba na staa wa zamani wa Simba na Yanga, Mganda Hamis Kiiza yalikuwa kama hivi:-

BINGWA: Ulianza kucheza soka ukiwa na umri gani?

Zakari: Nilianza kucheza soka nilipokuwa na umri wa miaka 12, safari yangu katika mchezo wa soka ilianza  katika kituo cha vijana cha Ajax nchini Ghana ambacho kilinilea katika misingi ya soka.

BINGWA: Nini kilikuvutia kujiunga Ajax na ulidumu kwa muda gani?

Zakari: Ni kituo kizuri na chenye vijana wengi, nilikaa misimu miwili baadaye nilijiunga na kituo cha Wanjire United nilipokuwa na miaka 14, ambapo nilianza kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi hicho mpaka nilipofikisha miaka 17 nikajiunga na klabu ya Union Sportive Doula ya Cameroon.

BINGWA: Ni changamoto gani ulikutana nayo mara baada ya kuhama na kwenda kucheza soka nje ya nchi?

Zakari: Changamoto zipo nyingi kwanza katika kikosi cha Union Sportive, mimi ndio nilikuwa mchezaji mdogo kuliko wote hivyo nilikuwa natumia nguvu nyingi ili kuendana na kasi ya wachezaji niliowakuta hapo.

BINGWA: Ni kitu gani huwezi kukisahau katika klabu ya Union Sportive Doula?

Zakari: Aina ya vyakula nilivyokutana navyo kule kama unavyojua kila nchi ina aina yake ya vyakula, hivyo ilinipa wakati mgumu sana kuzoea aina ile ya vyakula vya Cameroon.

BINGWA: Umewahi kuitwa katika kikosi cha timu ya Taifa au kikosi cha vijana?

Zakari: Ndio, nimewahi kuitwa mara moja katika kikosi cha taifa cha vijana cha Ghana mwaka 2014, tangu mwaka huo sijawahi kuitwa tena katika kikosi hicho kwa kuwa nilikuwa sina timu hivyo kocha hajaniona ndio sababu nimeamua kuja Tanzania kutafuta timu.

BINGWA: Mbali na Ghana na Cameroon, ni nchi gani nyingine umewahi kucheza ligi?

Zakari: Mara baada ya kuondoka Cameroon nilijiunga na klabu ya Nogoom el Mokhbal inayoshiriki Ligi Kuu ya Misri lakini nilishindwa kucheza kutokana na chama cha soka cha nchini kusema kila timu ipunguze nyota wa kigeni ndipo nilipopunguzwa.

BINGWA: Kabla ya kuja nchini ulikuwa unaijua Ligi ya Tanzania Bara?

Zakari: Ndio niliijua Ligi Kuu ya Tanzania hasa klabu kongwe za Simba na Yanga kupitia kwa rafiki yangu Hamis Kiiza ambaye tulicheza pamoja nchini Misri katika klabu ya Nogoom el Mokhbal lakini pia aliwahi kuzichezea timu hizi.

BINGWA: Mara baada ya kuondolewa nchini Misri ulijiunga na klabu gani?

Zakari: Baada ya kuondoka nchini Misri nilirudi nyumbani nchini Ghana na kuendelea kujifua katika kituo cha kukuzia vijana cha Ajax kulinda kiwango changu, niliamua kurudi Ajax kwa kuwa pale ni kama nyumbani kwani ndio kituo kilichonilea kisoka.

BINGWA: Hii ni mara yako ya ngapi kuja  hapa nchini?

Zakari: Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania nilikuwa nasikia tu kutoka kwa rafiki zangu ambao ni wafanyabiashara na wao ndio walionivutia mimi nije kujaribu bahati yangu.

BINGWA: Ni kitu gani kilikupa wakati mgumu ulipotua nchini?

Zakari: Lugha ndiyo inayonitesa sana kwani asilimia kubwa ya watu hapa wanaongea Kiswahili tofauti na Ghana ambapo tunatumia na Kiingereza.

BINGWA: Hadi sasa ni timu ngapi zimeonyesha nia ya kufanya kazi na wewe?

Zakari: Nimefanya mazungumzo na timu nyingi lakini iliyoonyesha nia ya kufanya kazi na mimi ni Stand United ambao kama mipango itakamilika huenda nikajiunga nao katika dirisha dogo la usajili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -