Tuesday, October 27, 2020

Azam FC hasira zote kwa Stand

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MAREGES NYAMAKA

BAADA ya kushindwa kutumia vema uwanja wa nyumbani wa Chamanzi Complex, uliopo Mbagala, Dar es Salaam kwa kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Ruvu Shooting, Azam wamepania kumaliza hasira zao kwa Stand United ya mkoani Shinyanga.

Sare hiyo waliyopata Azam kutoka kwa  Maafande hao wa mkoani Pwani  imewapelekea  kushika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakiwa na pointi zao 10, wakiwa wamecheza jumla ya michezo saba.

Akizungumza na Bingwa, Meneja wa Azam, Zacharia Alando, anaamini timu yao licha ya kuambulia pointi moja, bado timu yao ina nafasi kubwa ya  kufanya vizuri na tayari matokeo hayo wameyaweka pembeni wanaangalia mchezo ujao  wa ugenini dhidi ya Stand United, ambapo wana safiri kesho kuelekea mkoani Shinyanga

“Ni kweli si matokeo mazuri sana katika uwanja wa nyumbani, lakini ndo hivyo, hii ni ligi na kila timu imejiandaa vema kupambana, haijalishi ni uwanja wa nyumbani, lakini hata hivyo tunaangalia mchezo ujao dhidi ya Stand United, safari yetu ya kuwafuta  rasmi, maana utaratibu wetu wa mechi za mkoani tunaondoka  kati ya siku nne au tatu kabla,” alisema.

Wanalambalamba hao  hawajaonja ladha ya ushindi ndani ya mechi tatu sasa tangu walipofungwa na Simba bao 1-0 Uwanja wa Uhuru, na wiki moja baadaye wakabamizwa bao  2-1 dhidi ya Ndanda katika dimba la Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara, kabla ya sare ya juzi Jumapili 2-2 mbele ya Ruvu Shooting.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -