Thursday, December 3, 2020

AZAM FC KUTUMIA STAILI ILIYOMSHINDA HERNANDEZ

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA EZEKIEL TENDWA

KAA chonjo. Hivyo ndivyo unavyoweza kuziambia timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kocha mkuu wa Azam FC, Aristica Cioaba, kuweka wazi kuwa anataka soka kama Barcelona ya nchini Hispania.

Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo, kocha huyo raia wa Romania, alisema anataka kuiona timu hiyo ikicheza soka la kushambulia na kurudi kukaba kwa pamoja.

“Mimi ni kocha ninayependa soka la kushambulia, si aina ya kocha ninayependa timu yangu icheze kwenye eneo la kujilinda, napenda kuwapa mabao mengi mashabiki wanaokuja uwanjani kushuhudia mechi na kuwafanya baada ya mechi wawe na furaha,” alisema.

Aina hiyo ya soka analohitaji kocha huyo linaweza kufanana na lile linalopigwa na timu ya Barcelona ya Hispania, ambalo limekuwa mwiba mchungu kwa wapinzani wake na kuisaidia kutwaa vikombe mbalimbali vya ndani na nje ya nchi hiyo.

Aina hiyo ya soka iliwahi kutumiwa na Azam wakati ikifundishwa na mtangulizi wa Cioba, Zeben Hernandez, ingawa haikuletwa matunda mazuri hatua iliyopelekea atimuliwe.

Kwa sasa Azam ambao ni mabingwa wa michuano ya Mapinduzi wapo kwenye maandalizi kabambe kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mwadui FC kesho katika Uwanja wa Azam, Complex, Chamazi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -