Saturday, November 28, 2020

AZAM FC WASIRUDIE KOSA HILI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TIMU ya Azam inatarajia kuiwakilisha nchi katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika itakayoanza mwezi ujao.

Azam inatarajia kushiriki michuano huku wakiwa wametimua benchi lote la ufundi lililokuwa likiongozwa na kocha Mhispania Zeben Harnendez.

Tunaweza kuona uamuzi wa Azam ulikuwa sahihi wa kutimua benchi la ufundi baada ya kuona timu yao haifanyi vizuri Ligi Kuu Tanzania Bara.

Lakini Azam walichelewa kuchukua uamuzi huo kama walijua kuwa wanahitaji kuwa na benchi la ufundi ambalo litawapa mafanikio kwenye michuano ya kimataifa.

Kwa maana hiyo, Azam wataingia kwenye michuano hiyo wakiwa na benchi jipya la ufundi ambalo litakuwa lina muda mfupi sana wa kuwaandaa wachezaji na kuweza kuelewa mfumo wa kocha mkuu atakayeliongoza benchi hilo.

Tunaona muda uliobaki katika maandalizi ya michuano hiyo ya kimataifa ni mfupi mno ukizingatia kocha mpya atakuja na mfumo wake mwingine wa ufundishaji tofauti na ule uliokuwa unafundishwa na Zeben.

Pamoja na matarajio yetu kutaka Azam kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, lakini changamoto tunaiona mbele yao ni kocha mpya.

Kitendo cha Azam kutimua benchi la ufundi katikati ya msimu, sisi tunaona ni jambo la hatari wanaweza wakafanya vibaya kutokana na mfumo wa kocha mpya utakuwa ni mgeni kwa wachezaji.

Tunafahamu kwamba, Azam wamefanya kosa kubwa kuwaondoa makocha wote, lakini hatutarajii kuona wanafanya kosa jingine la kukurupuka kuleta kocha wa kigeni ambaye hana uzoefu wa soka la Tanzania na michuano ya Afrika ngazi ya klabu.

Uongozi wa Azam unatakiwa kutuliza akili na kufanya uamuzi sahihi wa kumleta kocha mwenye uzoefu mkubwa la Ligi ya Tanzania, lakini michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Tunaamini kwamba, ushauri wetu huu Azam watauzingatia kama wanataka timu yao kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Tunawakia kila la kheri katika mchakato wao wa kumleta kocha mpya ambaye ataleta mafanikio makubwa ndani ya klabu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -