MAREGES NYAMAKA NA TIMA SIKILO
LICHA ya timu ya Lipuli kuwa na wachezaji wengi wazoefu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam wamesema hawana presha ya kupata pointi tatu mbele yao katika mchezo utakaochezwa Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA, Meneja wa kikosi hicho, Philipo Alando, alisema kwa mujibu wa kocha wao, Aristica Cioaba, anaridhishwa na uwezo wa wachezaji wake.
Alando alisema kuelekea mchezo huo hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi.
“Wachezaji wana morali ya kupambana kusaka pointi tatu, ambapo leo (jana) tumeingia kambini, tunawaheshimu Lipuli wana kikosi kizuri chenye wachezaji wazoefu, naamini utakuwa mchezo wa kuvutia kwa pande zote mbili,” alisema.
Lipuli walitarajia kuwasili jana usiku jijini, ambapo kocha wa timu hiyo, Amri